December 18, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Tanzania yang’ara Uimara wa kiuchumi: IMF yathibitisha Tanzania kuimalika

Rais Samia Suluhu Hassan

 

Ripoti ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) kuhusu hali ya deni la mataifa 186 duniani imeonyesha kuwa Tanzania inazidi kuimarika kiuchumi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Katika ripoti hiyo ya Economic Outlook ya iliyotoka hivi karibuni, Tanzania imeorodheshwa na uwiano wa deni kwa uchumi wa asilimia 47%, kiwango kinachothibitisha usimamizi bora wa uchumi ukilinganisha na mataifa mengine ya Afrika na duniani kwa ujumla.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wastani wa deni kwa uchumi wa mataifa ya Afrika ni asilimia 67%. Hii inamaanisha kuwa Tanzania iko mbali chini ya wastani huo, hali inayoashiria uwiano mzuri wa kukopa na matumizi ya fedha za umma. Kulinganisha na majirani na washirika wengine wa maendeleo, takwimu zifuatazo zinajitokeza.

Kenya (70%), Rwanda: 71%, Uganda: 51%, Malawi: 84%, Msumbiji: 96%, Namibia: 67%, Ghana: 82%

Ikilinganishwa na takwimu hizi, ni dhahiri kuwa Tanzania imedhibiti deni lake vyema zaidi ya mataifa mengi yanayofanana nayo kiuchumi.

Rais Samia: Mchumi Anayeweka Misingi Imara; Tangu kuingia madarakani mwaka 2021, Rais Samia Suluhu Hassan ameonyesha dira na weledi wa kipekee katika usimamizi wa uchumi. Kupitia sera zake, serikali imeendelea kuweka mkazo katika matumizi yenye tija na kuwezesha miradi ya kimkakati ambayo inaleta tija moja kwa moja kwa wananchi.

Kwa mfano, miradi mikubwa kama reli ya SGR, bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere, na maboresho ya bandari yamefadhiliwa bila kufikia viwango vya hatari vya deni. Serikali pia imeboresha mazingira ya uwekezaji, hatua ambayo imeongeza mapato ya ndani na kupunguza utegemezi wa mikopo.

About The Author

error: Content is protected !!