MSANII wa muziki kutoka nchini Rwanda, Bruce Melodie, ameachia singo yake mpya iitwayo “Niki Minaji” akiwa amemshirikisha msanii wa Afrika Kusini, Blaq Diamond. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Ni kibao chenye mikong’osio ya Amapiano na Afropop ambapo wawili hao wamefanya vurugu za aina yake katika wimbo huo.
Wimbo huo haumzungumzii moja kwa moja Nicki Minaj kama binadamu bali unaelezea namna Nicki Minaj alivyo mrembo na mwenye kujiamini mbele ya jamii.
Ujumbe wa wimbo huo unaelezea namna mtu anapokuwa kwenye mapenzi na msichana mrembo ambaye pia ni maarufu kwenye jamii yake jambo linalompotezea kujiamini.
“Nilitaka kuonyesha kwamba unapokuwa katika mapenzi ya dhati, hata kama huyo mtu ni mrembo kiasi gani, mtanashati au jasiri, anaweza kulinganishwa na msichana huyu ninayempenda,” Bruce Melodie alizungumzia video hiyo iliyorekodiwa jijini Kigali, Rwanda, ikiongozwa na Jean Chretien Munezero.
Wakati huohuo, Bruce Melodie alitangaza kujiandaa kutoa kwa albamu yake mpya ya nne iitwayo ‘Colorful Generation’, ambayo itatoka mapema mwakani, 2025.
Ni albamu iliyowashirikisha mastaa kibao wakiwemo,Joeboy kwenye traki “Not A Lie” , Mkenya Bien kwenye wimbo “Iyo Foto” na staa wa kimataifa wa Reggae /dancehall, Shaggy kwenye wimbo “When She’s Around (Funga Macho)”.
ZINAZOFANANA
Moto wa Chelsea waendelea kuwaka huko Uingereza
Tusua na wakali wa ubashiri Jumapili ya leo
Harmonize agonga kolabo na mastaa kibao