Mahakama ya Katiba imetoa uamuzi kuwa, rais wa zamani wa Zambia, Edgar Lungu, hawezi kugombea tena urais kwa sababu ameshaongoza vipindi viwili vinavyoruhusiwa kisheria. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Lungu mwenye umri wa miaka 68 kwanza alichaguliwa kuongoza Januari 2015 kumalizia miezi 20 iliyosalia baada ya mtangulizi wake
Michael Sata kufariki dunia Oktoba 2014.
Lungu ambaye amechaguliwa na muungano wa Tonse kuwania urais 2026 aliitoa hoja kwamba kipindi hicho kisifikiriwe kwani hakutumikia kipindi kuzima cha miaka mitano. Lakini mahakama ilipinga hoja hiyo, hivyo ikabatilisha uamuzi wa awali ambao ulimsafishia njia kuwania muhula mwingine miaka mitatu baada ya kuangushwa na Hakainde Hichilema
ZINAZOFANANA
Kagame, Tshisekedi, uso kwa uso Dar es Salaam
Rais wa Sierra Leone awasili nchini
Dk. Mpango: Marekani ina mchango mkubwa katika maendeleo