KAMPUNI ya Serengeti Breweries Limited (SBL) inashirikiana na watu duniani kote kusherehekea Siku ya Kimataifa ya Watu Wenye Ulemavu inayoadhimishwa kila tarehe 3 Desemba ya mwaka, kumbukumbu muhimu ya kutetea haki, kuongeza uelewa, na kuimarisha ujumuishi kwa mamilioni ya watu wenye ulemavu duniani kote. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kaulimbiu ya mwaka huu, “Kuimarisha Uongozi wa Watu Wenye Ulemavu kwa Ajili ya Mustakabali Jumuishi na Endelevu,” inachochea uchukuaji wa hatua kwa kuonesha faida za kuwawezesha watu wenye ulemavu kwenye jamii.
SBL inakubaliana na maono haya, ikichochea mabadiliko kupitia programu na mashirikiano ya kibunifu yanayolenga kuinua na kuwawezesha watu wenye ulemavu hapa nchini.
Kampuni ya SBL imekuwa mstari wa mbele katika kuhimiza ujumuishi, ikihakikisha watu wenye ulemavu wanapewa nafasi ya kufanikiwa kama viongozi na wachangiaji katika kuleta maendeleo ya taifa. Moja ya mipango yenye faida zaidi ni programu yake ya kilimo biashara, ambayo mwaka huu imewapa mafunzo ya mbinu za kilimo cha kisasa watu 100 wenye ulemavu. Ujuzi huu umewawezesha washiriki kuboresha maisha yao, kusaidia familia zao, na kuchangia kikamilifu kwenye jamii zao.
“Programu hii si tu inahusu kilimo; inafungua fursa na kutambua talanta za uongozi. Kwa kuwapa watu wenye ulemavu ujuzi na fursa, tunawawezesha kuchukua hatamu ya uongozi na kufanya maamuzi juu ya maisha yao na hivyo kuchangia katika maendeleo ya taifa lao,” anasema John Wanyancha, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni wa SBL.
Ushirikiano na mashirika kama Sightsavers na Syngenta Foundation East Africa umeongezeka kwa kasi sana. Mwaka 2024, kuanzishwa kwa majaribio ya “farmer hub” mkoani Singida kuliwanufaisha wakulima wa mtama zaidi ya 200, wakiwemo watu wenye ulemavu. Kituo hicho kinatoa hudumu kama sehemu ya kupata mbegu bora, mbolea, na mafunzo kupitia shamba la mfano.
Zaidi ya kutoa nyenzo za vitendo, kituo hiki kimekuwa alama ya matumaini, kikikabiliana na unyanyapaa wa kijamii na kuimarisha mabadiliko ya tabia ya wakulima. Ushirikiano wa mara kwa mara kati ya wakulima umejenga mshikamano, imeimalisha usawa wa kijinsia, na kusaidia kupaza sauti za watu wenye ulemavu kwenye masuala ya kilimo.
“Vituo hivi ni zaidi ya mafundisho—ni alama ya matumaini na ujumuishi. Vinathibitisha kuwa msaada wa makusudi unaweza kusababisha mabadiliko ya kitabia na kujenga jamii jumuishi zaidi,” anaeleza Wanyancha.
Naye Michael Salali, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi inayotetea haki za watu wenye ulemavu, Foundation for Disabilities Hope (FDH), alipongeza juhudi za SBL katika kuwawezesha watu wenye ulemavu. “Programu kama hizi ni muhimu katika kubadilisha mitazamo kuhusu watu wenye ulemavu,” anasema.
“Kwa kutoa mafunzo, rasilimali, na majukwaa ya uongozi, SBL inathibitisha kwamba ujumuishi unaleta manufaa kwa kila mtu. Watu wenye ulemavu si mzigo; ni nguvu kubwa ya mabadiliko wanapopewa fursa sahihi.”
Salali pia alisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kuleta faida za muda mrefu. “Ni lazima tushirikiane—makampuni, serikali, na asasi za kiraia—kuhakikisha kila mtu, bila kujali uwezo
Kupitia mipango yake ya kibunifu, SBL inaamini kuwa ujumuishi si tu kanuni—ni vitendo vyenye nguvu za kubadilisha maisha ya kila mtu. Ahadi ya kampuni hiyo ya kuwawezesha watu wenye ulemavu inalenga kuleta mabadiliko kwa watu binafsi, familia, jamii, na taifa kiujumla.
Tunapoadhimisha siku hii muhimu, juhudi za SBL zinabaki kuwa mfano wa kuonesha faida zinazoweza kupatikana pale ujumuishi unapokuwa dhamira ya pamoja. Kwa kupingania ushirikishwaji na kuimarisha uongozi, tunaweza kujenga mustakabali unaosherehekea mchango wa kila mtu na kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma.
ZINAZOFANANA
Zungusha na ushinde katika Promosheni ya Mwezi wa Pesa
Black Gold kasino mgodi wa madini Meridianbet
Xmas Drop, zawadi kubwa zinazungumziwa!