Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza imemuachia huru aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk. Yahya Nawanda katika kesi ya kulawiti iliyokuwa inamkabili. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea).
Uamuzi wa kesi hiyo namba 1883/2024, umetolewa leo tarehe 29 Novemba 2024, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo Erick Marley.
Akisoma uamuzi huo, hakimu alisema kuwa baada ya kupitia ushaidi na vielelezo vilivyowasilishwa kwenye shauri hilo, Mahakama imejiridhishwa kuwa, hakukuwa na muunganiko wa ushahidi unaoweza kumtia mshtakiwa na kuamua kumuachia huru.
Dk. Nawanda alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza, tarehe 09 Julai 2024, na kosemewa shtaka hilo na waendesha Mashtaka wa Serikali, Magreth Mwaseba na Martha Mtiti.
Kwa mujibu wa Mwaseba alieleza Mahakama hiyo kuwa, mshtakiwa alidaiwa Kutenda kosa hilo tarehe 02 Juni 2024, kwenye eneo la maegesho ya magari lililoko Rock City Mall wilayani Ilemela mkoani Mwanza.
Aliendelea kusema kuwa Kutenda kosa hilo ni kinyume na kifungu namba 154 (1)(a) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16.
Mara baada ya kuachiwa huru na Mahakama hiyo, Dk Nawanda aliwaambia waandishi wa Habari kuwa, Mahakama imetwenda Haki hivyo anamshukuru Mungu.
“Namshukuru Mungu, Familia Yangu na Mahakama imetenda Haki, Mungu ni Mwema kila kitu kinatoka kwa Mungu, utukufu ni wake Mungu.”alisema Dk. Nawanda.
Watu 2,309 Wachaguliwa, Kuchaguliwa Bwana, Kuchaguliwa Huko
Vijiji 97, Mitaa 36, Tongoji 853, WajumbeH 1,222, WajumbeM 101 = 2,309
Jenga Nyumba ya Tembe Tuuu hapo gharama nguvu zako na Jasho na kaharufu ka mwili kidogo
Ndio maana tuwape hongera wananchi kwa kuwa..
Chadema ikishinda (Kimyaaaa mtaa wote kichekooo)
Chadema ikishindwa (Tumeibiwa kura – Hakuna uchaguzi kuna uchafuzi – Kura feki – Polisi wamewasaidia)
Inahitaji JESHI, Polisi, FBI (Kwa sababu ya watalii wanaokuja Zanzibar na Kilimanjaro – Watalii hawawezi kuja Tanzania kuangalia viazi utamu au machungwa ya Tanga), ICC, kujua aina ya Siasa zinazofanyika Tanzania
Hata malengo ya maendeleo endelevu wamekupiga bao la kisigino sema tu hawatakiwi kutangazwa