November 23, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Bunge laridhika na utekelezaji wa mitadi ya misitu na nyuki

 

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeridhika na miradi mbalimbali ya misitu na nyuki inayotekelezwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Mfuko wa Misitu na Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki Tabora (BTI) na kupongeza kwa kazi nzuri inayofanyika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tabora … (endelea).

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Timotheo Mnzava (Mb) ametoa pongezi hizo leo katika siku yake ya kwanza ya ziara ya kikazi mkoani Tabora wakati ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya sekta ya misitu na nyuki huku akitaka juhudi hizo ziongeze ili kukamilisha kabisa kazi zilizobaki kwa baadhi ya miradi.

Kamati imefika jana ambapo inaendelea kesho kwa mkoa wa Tabora na Singida imeambatana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dustan Kitandula (Mb), Katibu Mkuu, Dk. Hassan Abbasi na baadhi ya Watendaji wa Wizara na taasisi zilizo chini ya Wizara.

Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Deusdedith Katwale pia ameipongeza na kuishukuru Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuleta ubunifu na wa kuanzisha nembo (trade mark) maalum inayotambulisha asali kimataifa.

“Napenda kuishukuru na kuipongeza Wizara ya Maliasili na utalii kwa mapinduzi makubwa kwenye sekta hii kwa kuanzisha nembo ya asali yetu ambayo itasaidia kuitambulisha asali ya Tanzania kwenye masoko ya kimataifa hivyo kuuza asali kwenye masoko ya kimataifa tofauti na awali,” amefafanua Katwale

Katika miradi hiyo Mfuko wa Misitu Tanzania umetoa ruzuku kwa miradi 56 katika Mkoa wa Tabora pekee yenye thamani ya takribani Sh. 2.2 bilioni.

Miradi hiyo inatekelezwa katika Wilaya zote 7 za Mkoa wa Tabora ambazo ni Tabora, Uyui, Nzega, Igunga, Sikonge, Urambo na Kaliua.

Aidha, kati ya miradi hiyo ipo miradi ya ufugaji nyuki inayotekelezwa zaidi na vikundi vya kijamii, viwanda vya mazao ya nyuki na miradi ya kuimarisha Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji nyuki Tabora (BTI).

Pia Mfuko unagharamia ujenzi wa kiwanda na ununuzi wa mitambo kwa ajili mafunzo ya kuchakata na kufungasha mazao ya nyuki katika Chuo cha BTI kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi.

Kamati, pia imepata bahati ya kutembelea na kujionea mradi wa ukarabati wa jengo la utawala la Chuo, ujenzi wa jengo la karakana ya mbao kwa ajili ya kuwezesha utoaji wa mafunzo ya utengenezaji wa mizinga bora ya nyuki, ujenzi wa jengo la ukumbi wa mihadhara (lecture theatre) kwa matumizi wanafunzi wa BTI na Kituo cha ufugaji nyuki kibiashara kilianzishwa kama mkakati wa kuongeza kipato cha jamii kwa uboreshaji wa uchumi na kupunguza uharibifu wa misitu ya hifadhi katika Mkoa wa Tabora.

About The Author