November 6, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Mluya awachimba mikwara wasimamizi wa uchaguzi “atakavuruga tutashughulika naye’’

 

CHAMA cha DP kimetoa tahadhari kwa wasimamizi wa uchaguzi kusimamia uchaguzi na mchakato wake kwa haki endapo watavuruga uchaguzi huo hawatakubali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamesema leo tarehe 6 Novemba, 2024 na Abdul Mluya, Katibu Mkuu wa chama hicho, alipokuwa akizungumza na waandsishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa chama hicho hakitegemei mgombea wake ataenguliwa.

“Hatutegemei kuona mgombea wetu anaenguliwa hii nitoe angalizo kabisa kwa wasimamizi wa uchaguzi kwa sababu tumewapa mafunzo waofisa wetu na wamekwenda kusimamia fomu moja baada ya nyingine wanasema DP tunapenda kesi sasa tutaanza kuzifufua ikiwa tu mgombea wetu yeyeto ataenguliwa kwa sababu tunahakika asilimia mia moja fomu zimehakikiwa na maofisa wetu walipewa mafunzo vizuri kwa hivyo wasimamizi wa uchaguzi niwape onyo hiyo tarehe nane, tisa na 10 wajue kabisa kwamba kwenye fomu za DP hatutakuwa na masihala,” amesema Mluya.

Amesema kuwa ikitokea mgombea wa chama hicho ameshindwa kihalali watakubali lakini wakishindwa kwa dhulma hawatakubali: “Namna gani hatutakubali tutawaambia wakati huo hatuwezi kumuuzia adui silaha na tukishinda tutangazwe hili angalizi kwa wasimamizi wa uchaguzi wasiende kwenye uchaguzi kiushabiki waongozwe na taratibu za kanuni na sheria msimamizi yoyote atakayeharibu uchaguzi tutasimama na yeye kwanza kwa sababu hatuna imani kwamba mamlaka iliyomuweka pale ndio iliyomtuma aharibu uchaguzi isipokuwa ataharibu kwa utashi wake kwa sababu miongozo ya uchaguzi ipo hivyo tutashughulika naye binafsi.

Ametoa wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha hawaingilii uchaguzi huo badala yake walinde misingi ya haki.

Mluya ametoa tahadhari kwa viongozi na wagombea ndani ya chama chake na vyama vingine wakafanye siasa za kistaarabu.

Wakati huo huo ameeleza namna chama hicho kilivyojipanga kushinda uchaguzi huo: “Tumewasimamisha wagombea kwenye mikoa 14 hatukusimamisha wagombea kwa maana ya kushirki tunakwenda kushinda tunakwenda kurejesha ufulme wetu katika maeneo tuliyokuwa tunayatawala kabla ya uchaguzi ule wa kumbakumba na tuna kwenda kuongeza utawala wetu kwa sababu tunaimani wananchi walikuwa wakiisubiri DP muda mrefu na sasa ndio wakati wa chama chao kurudi kuongoza.

Ameitaja mikoa waliyoiweka kwenye ramani ya mkakati wao ikiwa pamoja na Arusha, Manyara, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kigoma, Mara , Manyara, Mbeya, Mtwara Mwanza, Morogoro, Songwe, Shinyanga na Tabaora.

About The Author