November 21, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

St Anne Marie Academy yafanya maajabu tena darasa la 7

 

SHULE ya St. Anne Marie Academy ya Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam, imeendelea kufanya maajabu kwenye mitihani ya darasa la saba ambapo mwaka huu wanafunzi wake 140 waliohitimu darasa la saba wamefaulu kwa alama A. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa shule hiyo, Gladius Ndyetabura wakati wa msafara wa shule hiyo kwenye maeneo mbalimbali wilaya ya Ubungo kusherehekea matokeo hayo.

Msafara wa magari 40 ya shule hiyo yaliyobandikwa matokeo ya shule hiyo mwaka huu yalizunguka maeneo mbalimbali za Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam wakiongozwa na gari la polisi na kuwa kivutio kwa watu wengi.

Ndyetabura amesema kwenye matokeo hayo yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), wanafunzi 140 wa shule hiyo wamepata wastani wa alama A na wanafunzi 15 tu ndiyo wamepata alama B.

“Tunasherekea matokeo ya darasa saba tulikuwa na wanafunzi karibu 150 na karibu wote wamefaulu kwa alama A tunawapongeza wanafunzi ambao wametuamini na kutupa watoto wao na tunaomba waendelee kutupa watoto wao kwasababu matokeo wameyaona,” alisema

Aidha, Ndyetabura ambaye pia ni mchambuzi wa masuala ya elimu aliwapongeza walimu wa shule hiyo kwa namna walivyokuwa wanapambana kuwafundisha wanafunzi hao usiku na mchana na hatimaye kupata matokeo mazuri ambayo ni ya kujivunia.

Alimpongeza Mkurugenzi wa shule za St Anne Marie Academy, Dk. Jasson Rweikiza kwa namna ambavyo amekuwa akiwawekea mazuri ya kufundishia iikiwemo maabara ya kisasa na maktaba yenye viyoyozi.

“Wanafunzi wa St Anne Marie Academy wanakula milo mitano kwa siku ni shule wachache sana zinazoweza kumudu kulisha wanafunzi wake mara tano kwa siku, tuna shamba laa mboga mboga kwaajili ya wanafunzi, tuna maji ya na umeme wa uhakika kwa hiyo tumekamilika tunamshukuru sana Dk Rweikiza,” amesema

Kuhusu siri ya mafanikio hayo, Ndyetabura alisema ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na Dk. Rweikiza katika miundombinu kama madarasa, mabweni, mabasi ya shule, maktaba iliyosheheni vitabu na walimu wenye weledi ambao wamekuwa wakifundisha kwa ari kubwa.

“Wakati NECTA ilipokuwa na utaratibu wa kutaja shule zilizokuwa zikifanya vizuri kitaifa tulikuwa tunashika namba nne, nafasi ya sita, nafasi ya nane na kuna wakati tulikuwa wa kwanza kitaifa na kwa matokeo haya tuliyopata mwaka huu kama wangetangaza huenda ungekuta tuko 10 bora kitaifa,” alisema

About The Author