November 22, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Waandishi Bora wa habari za Hali ya Hewa watunukiwa Tuzo

 

MWENYEKITI wa Bodi Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Jaji Mshibe Ali Bakari amewatunukia rasmi tuzo waandishi wa habari waliofanya vizuri kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2023 hadi Juni 2024 katika kuandika habari za hali ya hewa nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hafla hiyo fupi ilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Usafirishaji (NIT), Dar es Salaam, jana tarehe 28 Oktoba 2024.

Kabla ya kukadidhi tuzo hizo kwa washindi, Mshibe ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi wa hafla hiyo aliipongeza TMA kwa kuendelea kuwashirikisha na kutoa motisha kwa wanahabari katika utoaji elimu na usambazaji wa huduma za hali ya hewa

Alieleza kuwa, TMA ni moja ya taasis chache nchini, zinazothamini mchango wa wanahabari kwa ujumla ikiwemo ubunifu wa kuanzisha TUZO ya wanahabari bora wa habari za hali ya hewa nchini kwa miaka mitano sasa, ambapo kwa mwaka huu nimeelezwa kuwa TMA imeongeza wigo wa washindi.

Mwenyekiti wa Bodi Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Jaji Mshibe Ali Bakari

“Katika kuhakikisha tuzo hizi zinaendelea kuwa bora zaidi, mwaka huu Mamlaka imeboresha maeneo kadhaa ikiwemo kuongeza vipengele viwili vya waandishi kutoka nje ya Dar es Salaam na Zanzibar pamoja na kuboresha zawadi za washindi, hongereni sana TMA,” alisistiza Jaji Mshibe.

“Lengo kuu la Tuzo hizi ni kuendelea kuleta hamasa na kujenga umahili katika uandaaji na usambazaji wa tarifa za hali ya hewa kwa jamii, na kuimarisha mchango wa wanahabari katika kuelimisha jamii kuhusu umuhimu na matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa,” alieleza Jaji Mshibe

Akimkaribisha mgeni rasmi kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu, TMA, Dk. Hamza Kabelwa, Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri alisema Mamlaka kwa kutambua mchango huu mkubwa, imeendelea kuimarisha mahusiano haya kwa kuendelea kutoa motisha mbalimbali kwa wanahabari ikiwemo kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa takribani miaka 15 sasa hususani kipindi cha maandalizi ya utabiri wa mvua za misimu.

“Mafunzo haya yamekuwa yakitolewa, vilevile, kutafuta fursa za ushiriki wa waandishi wa habari kwenye mafunzo au majukwaa ya kimataifa mfano; Mwaka jana waandishi wa habari 10 walipata mwaliko wa kushiriki

About The Author