SERIKALI imepanga kutumia Sh. 379.3 bilioni kwa ajili ya ukarabati wa reli yenye urefu wa kilomita 210 kutoka Kaliua, Tabora hadi Mpanda Mkoani Katavi, pamoja na ujenzi wa njia ya kilomita 8 kwa ajili ya treni kupishana. Anaripoti Mwandishi Wetu, Katavi … (endelea).
Akizungumza na Wananchi wa Kata Ugalla katika ziara yake ya kikazi tarehe 27 Oktoba 2024, Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameidhinisha kiasi hicho cha fedha ili kuboresha huduma za usafiri na kuchochea maendeleo katika maeneo husika.
Amesisitiza kuwa wafanyakazi watakaoshiriki katika mradi huo watakuwa ni kutoka jamii ya Ugalla.
Katika ziara hiyo, Waziri pia amezindua miradi mingine, ikiwemo ujenzi wa mabweni mawili ya shule ya Sekondari Ugalla River na mradi wa maji wa Kabuga na Bulembo ambao umegharimu Sh. 1.4 bilioni na unatarajiwa kunufaisha wakazi wapatao 16,871 katika eneo hilo.
ZINAZOFANANA
Wafugaji watamba kuwaweka viongozi wa wilaya mfukoni
Mateso ya wazabuni Liwale, 15 wadhulumiwa malipo fedha zao
Waandishi Bora wa habari za Hali ya Hewa watunukiwa Tuzo