September 19, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Exim Bank yatoa vitanda vya wajawazito mkoani Morogoro

 

Katika kusaidia jamii na kuboresha huduma za afya nchini, Exim Bank Tanzania imetoa vitanda vya hospitali kwa wodi za wazazi katika Mkoa wa Morogoro. Makabidhiano hayo yamefanyika mbele ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ikiwa ni sehemu ya mapambano ya kupunguza vifo vya wamama na watoto wakati wa kujifungua.

Benki ya Exim Tanzania imekuwa ikishiriki katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo na kijamii katika sekta za mazingira, elimu, uchumi, utalii, michezo, na afya. Kwa mjibu wa taarifa za wizara ya afya, Serikali ya Tanzania imefanikiwa kupunguza vifo vya kina mama na watoto kutoka 556 mwaka 2016 mpaka kufukia vifo 104 mnamo mwaka 2023 ingawa bado hali sio salama sana.

Kwa kutambua changamoto hii pamoja na zingine zikiwemo uhaba wa vifaa vya matibabu, upungufu wa vitanda, madawa, na uchache wa watoa huduma za afya, benki ya E xim inaona ina nafasi kama taasisi kusaidia Serikali kupunguza tatizo la vitanda vya wajawazito.

About The Author