MJUMBE maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Dk. Lazarus Chakwera, tayari amewasili nchini. Anaripoti Saed Kubenea, Dar es Salaam … (endelea).
Taarifa za kuwasili nchini kwa rais wa zamani wa Malawi, kulitangazwa kwa mara ya kwanza na gazeti dada la MwanaHALISI, likinukuu vyanzo mbalimbali serikalini, balozi za Uingereza na Malawi jijini Dar es Salaam na serikali mjini Lilongwe.
Dk. Chakwera amekuja nchini, kumwakilisha Katibu Mkuu wa Commonwealth, Shirley Ayorkor Botchwey, kushughulikia mgogoro wa kisiasa, uliyotokana na uchaguzi mkuu wa 29 Oktoba mwaka jana.
Dk. Chakarwe ameteuliwa na Jumuiya ya Madola kuwa mwalikishi wake maalum wa kushughulikia mgogoro huo na serikali ya Tanzania, imeagizwa “kutekeleza masharti yote,” ili kujinusuru na kusimamishwa uanachama.
Katika uchaguzi mkuu wa 29 Oktoba mwaka jana, mamia ya watu wameripotiwa kufariki dunia kwa risasi za moto na wengine kadhaa kujeruhiwa na baadhi yao, maiti zao hazikupatikana.
Dk. Chakwera, aliwasili jana usiku, tarehe 08 Aprili 2026, kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ngwaru Maghembe.
Kwa habari zaidi, soma gazeti la MwanaHALISI, Alhamisi hii – Mhariri.
ZINAZOFANANA
Mwaka mmoja wa Lissu gerezani
LATRA yaongeza siku za maoni kuongeza bei
Jaji mstaafu Chade: Hatuna dalali