April 8, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

LATRA yaongeza siku za maoni kuongeza bei

Spread the love

 

MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA), imeongeza wiki mbili zaidi za kupokea maoni kutoka kwa wadau wa usafirishaji, kuhusu mapitio ya nauli baada ya bei ya mafuta kupandaji nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa LARTA, Dk. Habibu Suluo, tayari bei ya mafuta imeanza kushuka, hivyo baada ya muda wa kupokea maoni kukamilika, watapata picha ya hali inavyokwenda.

Bei ya mafuta nchini ilianza kupanda kwa kiwango kikubwa tarehe 1 Aprili mwaka huu.

Taarifa ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), ilieleza kuwa ongezeko hilo la bei, limechochewa na mgogoro wa kimataifa kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, uliyoanza tarehe 28 Februari 2026.

EWURA imesema, mgogoro huo umeathiri uzalishaji na usafirishaji wa mafuta ghafi ulimwenguni, hasa baada ya kufungwa kwa mlango wa Hormuz, unaopitisha takribani asilimia 20 ya mafuta yote duniani.

Aidha, kushambuliwa kwa visima vya mafuta, maghala ya kuhifadhi mafuta na viwanda vya kuyasafisha, kumeigusa moja kwa moja Tanzania, ambayo inaagiza mafuta kwa kiasi kikubwa, kutoka eneo la Mashariki ya Kati.

Serikali nchini Tanzania imetangaza bei mpya ya juu ya mafuta inayoanza kutekelezwa hii leo Jumatano tarehe mosi Aprili 2026.

Kulingana na EWURA, bei ya lita ya petroli jijini Dar es Salaam, imepanda kwa Sh. 956 (dola senti 37); kwa kufuata bei hiyo mpya, petroli inauzwa Sh. 3,820, dizeli Sh. 3,806 na mafuta ya taa yakiuzwa kwa Sh. 3,684.

Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania na mchumi Zitto Kabwe ameitaka serikali kuwasaidia wananchi kubeba mzigo huo wa mafuta.

Katika chapisho lake la mtandao wa X zamani Twitter Zitto alisema, “Leo tumeamka na bei mpya ya mafuta, bei tuliyoitegemea kufuatia mashambuliizi yanayoendelea ya Marekani na Israel dhidi ya Iran. Kama ilivyo sehemu zote duniani bei imepanda sana na gharama za maisha zitakuwa kubwa sana. Serikali isaidiane na wananchi kubeba gharama hizi.”

Kupanda kwa bei ya usafirishaji kunakoweza kufanywa na LATRA, kunataja na wachambuzi wa masuala ya kisiasa, kuwa kutachangia kwa kiwango kikubwa ongezeko la ugumu wa maisha nchini.

About The Author

error: Content is protected !!