March 30, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Ibada ya kuuga mwili wa Marehemu Lukuvi mkoani Iringa

Spread the love

 

IBADA ya Misa ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) na Mbunge wa Jimbo la Isimani, William Lukuvi, imefanyika katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu, Kihesa mkoani Iringa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Iringa … (endelea).

Ibada hiyo imeongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Iringa, Romanus Mihali, na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Vyama vya Siasa, Viongozi wa dini pamoja na waombolezaji kutoka maeneo tofauti ndani na nje ya mkoa wa Iringa.

Katika hali ya huzuni na tafakari, waombolezaji walikusanyika kumuombea marehemu na kutoa heshima za mwisho, wakikumbuka mchango wake mkubwa katika uongozi na utumishi wa umma.

Ibada hiyo ilitawaliwa na utulivu na majonzi, huku wengi wakieleza kuwa maisha ya marehemu yanaendelea kuacha alama kupitia kazi na huduma aliyoitoa kwa Taifa.

William Lukuvi alifariki dunia tarehe 25 Machi 2026, katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu. Anatarajiwa kuzikwa kesho katika kijiji cha Idodi, Wilayani Iringa, huku taratibu za mwisho za mazishi zikiendelea kufanyika.

About The Author

error: Content is protected !!