BEI ya mafuta duniani imepanda kwa kasi huku hifadhi zikishuka kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari leo Jumatatu asubuhi, 30 Machi 2026 kufuatia kuongezeka kwa mvutano unaoendelea Mashariki ya Kati. Inaripot Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Reuters na BBC masoko yanaonyesha kuwa mafuta ghafi aina ya Brent yamepanda kwa zaidi ya asilimia tatu na kufikia zaidi ya Dola za Marekani 115 (Sh297,849) kwa pipa, huku mafuta yanayouzwa nchini Marekani yakipanda hadi Dola za Marekani 103 (Sh266,769) baada ya kuimarika kwa asilimia 3.5.
Wakati huohuo, masoko ya hisa barani Asia yameshuka kwa kiwango kikubwa, yakionyesha wasiwasi wa wawekezaji kutokana na hali ya kisiasa na kiusalama.
Fahirisi ya Nikkei 225 ya Japan imeshuka kwa asilimia 4.5, huku Kospi ya Korea Kusini ikiporomoka kwa asilimia nne.
Aidha, Serikali imesema Tanzania ina hifadhi ya mafuta yanayoweza kutumiwa kwa miezi mitatu kuanzia Mei hadi Julai mwaka huu, huku ikiweka bayana kuwa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ndiyo litakalo sambaza mafuta kwa kipindi hicho.
Hiyo ni baada ya TPDC kupata wasambazaji wenye uwezo wa kuleta mafuta kwa gharama nafuu kuliko wale waliopatikana kupitia Wakala wa Ununuzi wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA).
ZINAZOFANANA
Polisi wakana maafa mgodi wa Msasa, Geita
Ibada ya kuuga mwili wa Marehemu Lukuvi mkoani Iringa
NBC yaendesha kongamano maalum ‘Kuwanoa’ Wanawake Kiuchumi