March 18, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Kilimanjaro yazindua kampeni mpya ya ‘Vyakwetu Vizuri’

Alphonce Simbu

KILIMANJARO Premium Lager inatarajia kuzindua rasmi kampeni yake mpya ya ijulikanayo kama “Vyakwetu Vizuri” kwenye wikiendi ya Kilimanjaro Marathon, tukio litakalogeuza mashindano hayo maarufu kuwa jukwaa la kuonesha fahari, utamaduni na umoja wa Watanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kupitia kampeni hii, Kilimanjaro Premium Lager inaendelea kusimama kama nembo ya utambulisho wa Mtanzania kwa kusisitiza maadili, hekima, asili na mshikamano unaowaunganisha Watanzania pamoja. Huu ni wakati wa kuwaleta watu pamoja kusherehekea mafanikio na kuonesha taswira halisi ya Tanzania.

Kwa zaidi ya miaka 20, Kilimanjaro Premium Lager imekuwa mdhamini mkuu wa mbio za kilomita 42 za Kilimanjaro Marathon, ikiendeleza dhamira yake ya kudumisha umoja, mafanikio, ukarimu na uzalendo. Kwa sasa, marathon hii imekua zaidi ya mashindano ya riadha na kuwa tukio kubwa la kijamii na kitamaduni linalowaleta pamoja wanariadha, jamii na wageni kutoka ndani na nje ya nchi.

Kwenye kilele cha Kili Marathon mwaka huu, burudani itaongezeka kupitia Kili Dome, tamasha la siku mbili litakalofanyika kuanzia Jumamosi hadi Jumapili. Washiriki na mashabiki watapata fursa ya kufurahia muziki wa wasanii mbalimbali, vyakula vya asili, pamoja na shughuli mbalimbali za kiburudani zitakazofanyika.

Taarifa za Tiketi:

  • Tiketi za awali: TSh 20,000

  • Mlangoni: TSh 30,000

  • VIP: TSh 3,000,000 (kwa watu 10)
    Tiketi pia zitapatikana eneo la Moshi Golf Club kuanzia saa 10 jioni siku ya tukio. Watu wanashauriwa kuwahi mapema.

Ratiba ya Wasanii

Jumamosi, 21 Machi 2026:
Scotts Maphuma
Ali Kiba
Ciza
Joh Makini
Tllogi_M

Jumapili, 22 Machi 2026:
Adekunle Gold
Mbosso
Maphorisa
D Voice
Tllogi_M

Kiini cha kampeni ya “Vyakwetu Vizuri” kinatokana na methali na misemo ya Kitanzania ambayo imekuwa ikipitishwa kutoka kizazi hadi kizazi. Methali hizi zinaakisi maisha ya kila siku ya Mtanzania uvumilivu, umoja, ukarimu na nguvu ya kushirikiana.

Ili kuleta uhalisia wa kampeni hii, kutakuwepo na chupa maalum za toleo la kipekee zenye mgawanyiko wa methali. Watumiaji watahamasishwa kuunganisha methali hizo ili kukamilisha, ishara ya kuonesha kuwa nguvu ya Mtanzania ipo kwenye umoja.

Akizungumza kuhusu kampeni hiyo, Mkuu wa Masoko wa Tanzania Breweries Limited, Khensani Mkhombo, alieleza kuwa kampeni hii imejengwa juu ya utamaduni wa kila siku wa Mtanzania.

“Vyakwetu Vizuri ni kusherehekea hekima iliyopo kwenye utamaduni wetu. Methali zetu zinatuongoza namna ya kuishi, kupokea wageni na kusonga mbele pamoja. Kilimanjaro Marathon ni nafasi muhimu inayotuunganisha sote, na kampeni hii inaenzi umoja huo.”

Kampeni hii pia itamshirikisha mwanariadha maarufu wa mbio ndefu, Alphonce Simbu, ambaye ameipeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa.

Kama sehemu ya maadhimisho hayo, Simbu ataongoza utaratibu maalum wa kuwapa motisha wakimbiaji wa kilomita 42 kupitia wimbo wa hamasa utakaowasaidia kuendelea kupambana hadi mwisho wa mbio.

Akizungumzia uzoefu wake, Simbu alisema: “Nimepitia changamoto nyingi, lakini sikuwahi kukata tamaa. Nimejifunza kuwa ukiwa na nia, unapata njia. Hiyo ndiyo nguvu ya Mtanzania tunasimama pamoja, tunapambana, na tunaendelea kuonesha dunia uwezo wetu.”

Wakati wakimbiaji wakijiandaa kukimbia chini ya Mlima Kilimanjaro, kampeni ya “Vyakwetu Vizuri” inalenga kuwakumbusha Watanzania kuwa nguvu yao ya kweli ipo katika umoja, uthubutu na mshikamano wao.

About The Author

error: Content is protected !!