Jesca Magufuli
JESCA Magufuli, mtoto wa Hayati Rais Dk John Pombe Magufuli, amesema katika Mataifa mengine uwezo wa kiongozi haupimwi kwa mda aliokaa madarakani bali kwa alama walizoziacha katika maendeleo na mwenendo wa Taifa lake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Geita … (endelea).
Akitoa salamu kwa niaba ya familia leo tarehe 17 Machi 2026 kwenye Misa Takatifu ya kumbukizi ya miaka mitano (5) ya kifo cha Hayati Dk. John Pombe Magufuli, amesema wamekusanyika kukumbuka maisha na urithi wa kiongozi ambaye alitoa sehemu kubwa ya maisha yake kulitumikia Taifa lake.
“Ni miaka mitano imepita tangu Taifa kupokea habari ya kuondokewa naye lakini katika historia ya Jina la Dk John Magufuli limebaki kuwa sehemu ya historia ya Tanzania na Afrika kwa ujumla”
Amesema leo tunapomkumbuka hatumkumbuki kama baba yetu wa familia bali kama mmoja wa viongozi waliobeba kwa uzito mkubwa jukumu la kuimarisha misingi ya maendeleo ya Taifa letu
Aidha ametoa shukrani kwa niaba ya familia kwa serikali ya jamhuri ya muuungano wa Tanzania kwa namna ambavyo inaendelea kuhifadhi Kumbukumbu za hayati Dk Magufuli kwa heshima na staha inayostahili
ZINAZOFANANA
Radi yaua wanafunzi watatu Dar
RITA yawapiga msasa wajumbe Bodi mpya ya wadhamini Kanisa la Waadventista Wasabato
CCBRT yarejesha furaha kwa wenye matatizo ya macho Dar