Soko la kimataifa la michezo ya kubahatisha linaendelea kukua kwa kasi, na sasa limepata habari kubwa baada ya Expanse Studios kutangaza rasmi ushirikiano mpya na jukwaa maarufu la ubashiri duniani, Stake. Hatua hii inaashiria hatua nyingine muhimu katika safari ya Expanse ya kupanua ushawishi wake duniani, huku ikiwaletea wachezaji burudani mpya na michezo ya kisasa zaidi katika majukwaa makubwa ya ubashiri.
Expanse Studios ijulikana kwa ubunifu wake katika uundaji wa michezo inayotoa msisimko wa kipekee kwa wachezaji. Michezo kama Super Heli, Wild Icy Fruits, na VASO Psycho imekuwa maarufu katika majukwaa mengi ya ubashiri duniani, ikivutia wachezaji kutokana na ubunifu, teknolojia na burudani isiyoisha.
Expanse Studios ni sehemu ya familia ya Meridian Holdings Inc., kundi lenye nguvu linalosimamia chapa kadhaa za kimataifa katika tasnia ya michezo na burudani. Ndani yake pia kuna Meridianbet Group inayofanya kazi katika masoko mengi duniani, pamoja na RKings nchini Uingereza, Mexplay nchini Mexico na Classics for a Cause nchini Australia, jambo linaloonyesha ukubwa wa mtandao wa biashara uliopo ndani ya Meridian Holdings.
Akizungumzia makubaliano hayo, Mtendaji Mkuu wa Expanse Studios, Damjan Stamenkovic, alisema kuwa ushirikiano na Stake ni hatua muhimu katika mkakati wa kampuni hiyo wa kupanua usambazaji wa michezo yake Duniani. Alieleza kuwa kupitia miundombinu ya Hub88, Expanse itaweza kuwafikia wachezaji wengi zaidi wa kimataifa na kuongeza nguvu ya chapa katika soko la michezo ya kubahatisha.
Ikiwa na zaidi ya washirika 1,300 duniani pamoja na mkusanyiko wa zaidi ya michezo 70 ya kipekee, Expanse Studios inaendelea kujidhihirisha kama moja ya kampuni zinazoongoza katika ubunifu wa michezo ya kubahatisha. Ushirikiano na Stake unaashiria mwanzo wa sura mpya ya ukuaji, ambapo wachezaji wataendelea kufurahia michezo yenye ubora wa juu.
ZINAZOFANANA
Wild Easter Eggs inagawa ushindi mkubwa ndani ya Meridianbet Pasaka hii
Serikali yajipanga kutatua changamoto za mazingira ya biashara
TVBET ndani ya Meridianbet ikileta kasi, na burudani ya kasino isiyo na kikomo