March 16, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Balozi Nchimbi kuongoza miaka mitano ya kifo cha Magufuli

 

MAKAMU wa Rais wa Tanzania, Emmanuel Nchimbi, amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Chato Airport mkoani Geita Region leo tarehe 16 Machi 2026, ambapo alipokelewa na kusalimiana na viongozi mbalimbali wa serikali na chama. Anaripoti Mwandishi Wetu, Chato … (endelea).

Makamu wa Rais anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya kumbukizi ya miaka mitano ya kifo cha Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania, hayati John Pombe Magufuli. Maadhimisho hayo yatafanyika kesho tarehe 17 Machi 2026 katika Wilaya ya Chato District mkoani Geita Region.

Tukio hilo linatarajiwa kukutanisha viongozi wa serikali, vyama vya siasa pamoja na wananchi mbalimbali kwa ajili ya kumkumbuka na kutathmini mchango wa hayati Dk. Magufuli katika maendeleo ya taifa.

About The Author

error: Content is protected !!