Tundu Lissu akiwa mahakamani
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amefikishwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala Ndogo ya Dar es salaam kwa ajili ya kusikilizwa kwa hoja za maombi yake ya kutaka kujumuishwa katika kesi ya mgawanyo wa rasilimali za Chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Maombi ya Lissu yanatokana na kesi ya msingi iliyofunguliwa na Mwenyekiti mstaafu wa Chadema, Said Issa Mohammed pamoja na Wajumbe wawili wa Bodi ya Wadhamini wa Chama hicho kutoka Zanzibar ambao ni Ahmed Rashid Khamis na Maulida Anna Komu.
Shauri hilo linasikilizwa mbele ya Jaji Hamidu Mwanga ambapo katika kesi ya msingi, Walalamikaji wanadai kuwa kumekuwa na mgawanyo usio sawa wa mali na rasilimali za kifedha za Chama kati ya Zanzibar na Tanzania Bara jambo ambalo wanadai linakiuka sheria ya Vyama vya siasa pamoja na Katiba ya Chadema.
ZINAZOFANANA
Prof. Kabudi amrihi Lukuvi, Mgombea Mwenza wa NCCR- Mageuzi, azawadiwa ubunge
Mwigulu awahakikishia Wana-Isimani kukamilisha miradi iliyoachwa na Lukuvi
Tume ya Uchunguzi matukio ya Oktoka 29 kufikia kikomo Aprili 3