SHIRIKA la ndege la Air Tanzania Company Limited limetangaza kuendesha safari maalum ya ndege kati ya Dar es Salaam na Dubai siku ya Jumapili, 8 Machi 2026 kwa ajili ya kusaidia abiria walioathirika na kusimamishwa kwa safari za kawaida katika njia hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kwa mujibu wa taarifa ya shirika hilo, ndege hiyo itafanya safari ya Dar es Salaam – Dubai – Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya mpango maalum wa kuwarejesha abiria waliokwama kufuatia kusitishwa kwa safari za kawaida za njia hiyo.
Air Tanzania imeeleza kuwa safari hiyo ni maalum ya kuwarejesha abiria (repatriation flight) na haitakuwa safari ya kawaida ya kibiashara kama zilivyo safari nyingine za shirika hilo.
Aidha, shirika hilo limesema kipaumbele kitapewa abiria wenye tiketi halali za safari za awali za njia ya Dar es Salaam kwenda Dubai ambazo ziliathirika kutokana na kusimamishwa kwa safari hizo.
Abiria wanaohusika wameshauriwa kuwasiliana na ofisi za Air Tanzania kwa maelezo zaidi pamoja na kuthibitisha safari zao kabla ya kuondoka ili kuepuka usumbufu.
ZINAZOFANANA
Vanillah apata shavu Apple Music
Waziri wa Fedha awaongoza wateja, wadau wa NBC futari maalum Dar
BAKWATA: Wapuuzeni wanaokashifu Uislamu