February 28, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Nchimbi akemea magomvi ya kivyama

 

BALOZI Emmanuel Nchimbi, makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano amesema, hafurahishwi na magomvi yanayoendelea kati ya chama chake – Chama Cha Mapinduzi na upinzani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza kwenye msiba wa Askofu wa Kanisa Katoliki, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, leo Jumamosi, tarehe 28 Februari 2026, Balozi Nchimbi amesema, moja ya mambo ambayo yanamchukiza, ni ugomvi wa baina ya vyama.

“Sote tunajenga taifa moja, hakuna sababu ya kuwepo kwa mambo hayo,” alisema na kuongeza kwamba amekuwa na msimamo wa kutopenda mambo hayo na aliuonyesha hata alipokuwa katibu mkuu wa CCM.

“Mimi hata mambo ya kugombana kivyama vyama siyapendi; ni ujinga tu, nchi yenu moja mnagombana nini,” alihoji mwanadiplomasia huyo.

Amesisitiza kuwa hata mtu akihama kwenda chama kingine, hakuna shida kwa kuwa wote wanadhamira ya kulitumikia taifa.

Kardinali Pengo, aliyekuwa Askofu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, alifariki dunia, usiku wa kuamkia 20 Februari 2026, katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), wakati akiwa matibabu.

Mwili wake utazikwa leo, tarehe 28 Februari, ndani ya Kanisa mahali pa Hija ya Bikira Maria, katika kituo cha Pugu, jijini Dar es Salaam – kituo  ambacho alikifungua wakati wa uhai wake, tarehe 7 Julai 1995.

About The Author

error: Content is protected !!