GERSON Msigwa, Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, amesema meli inayokamatwa na madawa ya kulevya aina ua kokeni, nchini El Salvador, ilisajiliwa visiwani Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msigwa
Amesema, kufuatia tukio hilo serikali ya Zanzibar imechukua hatua ya kuifutia usajili meli hiyo.
Alisema, tarehe 18 Februari, serikali ya Zanzibar ilifuta usajili wa meli hiyo, FMS EAGLE, na hivi sasa haina usajili wa Zanzibar tena.
“Serikali ya Zanzibar imewatafuta wamiliki wa meli ili kujua kulikoni, lakini ushirikiano haujawa mzuri sana”, alisema serikali imeipiga kampuni ya meli kiasi cha dola za Marekani elfu ishirini, kwa mujibu wa taratibu za IMO .
Katika taarifa yake amesema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kufanya mawasiliano kupitia “wizara yetu ya mambo ya nje ili kuondokana na utambuzi wowote wa meli hii kimataifa… lakini zaidi ya hapo,inaendelea kufanya tathimini ya mawakala wote ambao wameingia nao mkataba wa kusajili meli ili wale ambao ni wababaishaji waondolewe kwenye orodha ya wasajili”
Msigwa amesema kwasababu imevunja taratibu, serikali ya Zanzibar tayari imekwishaanza kuchukua hatua na baadaye watatoa taarifa rasmi kuhusu hatua nyingine ambazo imechukua kuhusiana na sakata hilo.
Meli ya FMS Eagle yenye usajili wa Tanzania ilikamatwa El Salvador ikiwa na tani 6.6 za dawa za kulevya. Watu 10 kutoka Colombia, Nicaragua, Panama na Ecuador walikamatwa wakitarajiwa kufikishwa mahakamani.
Haijaelezwa dawa hizo zilikuwa zikitoka wapi na kuelekea wapi.
ZINAZOFANANA
Wamekimbilia Mahakama ya Rufani ili kumkomoa Lissu, haikubaliki kisheria
RITA yavunja bodi ya wadhamini Kanisa la Waadventista Wasabato
Kesi ya Lissu yasimama, Serikali yakimbilia Mahakama ya Rufaa