Tundu Lissu akiwa mahakamani
TUNDU Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anaanza kumuuliza maswali ya dodoso (cross examination), shahidi wa 14 ambaye ni shahidi wa siri aliyetambulishwa kama P9 ambaye ni mkazi wa Mbeya mjini aliyetoa ushahidi wake katika mahakama kuu kuwa alikuwa akihamasisha watu kuzuia uchaguzi mkuu wa mwaka jana. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Shauri hilo linalosikilizwa na jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji Jaji Dustan Ndunguru akishirikiana na Jaji James Karayamaha na Jaji Ferdinand Kiwonde.
Leo tarehe 20 Februari Lissu ameenza kumuuliza shahidi huyo kutokana na ushahidi aliouwasilisha katika Mahakama Kuu, Masjala ndogo ya Dar es Salaam.
Lissu: Waeleze majaji kama uliandika maelezo tarehe 22 Aprili 2025?
Shahidi P9: Ndio.
Lissu: Waeleze majaji kama ukionyeshwa maelezo hayo utayatambua?
Shahidi P9: Ndio nitayatambua. (Anapelekewa maelezo yake).
Lissu: Waeleze majaji kama hayo ndio maelezo yako uliyoandika polisi tarehe 22 Aprili 2025?
Shahidi P9: Ndio ni yenyewe.
Lissu: Sasa shahidi umesikia nilichokisoma, waeleze waheshimiwa majaji kama nilichokisoma ndicho kilichopo kwako.
Sasa nataka nikueleze maeneeo nayotaka nikuhoji;-
1. Jana ulisema wewe ni mkazi wa Mbeya mjini, nataka nikuhoji hapo.
2. Kwamba wewe kazi yako ni fundi umeme na unafanya kazi ndani ya maeneo ya Jiji la Halmashauri ya Mbeya.
3. 2024 ulivutiwa na sera za Chadema na ukaamua kuwa mfuasi na ukawa unafatilia kwa karibu mikutano, matangazo na hotuba za viongozi wa Chadema.
4. Ulizungumzia matembezi ya amani yaliyofanyika Mbeya 2024 na ukasema Mbowe alianzia Songwe na Lissu Uyole na Heche Isanga.
5. Tarehe 3 Aprili 2025, ukiwa nyumbani kwako ulikua unaperuzi mitandao ya kijamii kwa simu aina Samsung 8 pro nataka nikuhoji kuhusu hiyo simu.
6. Uliingia kwenye mtandao wa Instagram na ili uingie kwenye mtandao huo lazima uwe na account na simu janja na bando ili kuweza kuangalia picha na video.
7. Wakati unaperuzi mtandao wa instagram uliona video ya Tundu Lissu lakini umesahau ilikua ni akaunti ya nani.
8. Huyo Lissu uliyemuona alikua amevaa kombati ya kaki za Chadema na tshirt nyeusi na alikua ukimbini na kulikua na bendera ya taifa na rangi za bendera ya Chadema.
9. Alisema tutavuruga uchaguzi kwa kufanya vurugu na kuvuruga uchaguzi huo.
10. Lissu alisema lazima tukichafue.
11. Ulipofika kwenye Kituo cha Polisi Mwanjelwa walikwambia wanataka wakufanyie tena mahojiano.
12. Nilihojiwa na mtu mmoja na mwingine wa pili alinihoji kwenye maswali mbalimbali.
13. Wakati unamjibu huyo anae kuhoji kwa mara ya pili niliona video ya Tundu Lissu, ndio nikaanza kufanya makosa.
Lissu: Sasa shahidi waeleze majaji kama ungependa maelezo yako yaingie kama kielelezo mahakamani?
Shahidi P9: Haina shida.
Upande wa Jamhuri: Hatuna pingamizi.
Mahakama: Yamepokelewa kama kielelezo D13
Iteendelea….
ZINAZOFANANA
Maandalizi ya kung’oa Lipumba yakamilika
Kardinali Pengo afariki Dunia
Mahkama Z’bar yatupa kesi za uchaguzi