ASKOFU Mkuu mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amefariki dunia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Askofu Pengo amefariki dunia usiku wa tarehe 19 Februari 2026 majira ya saa 4:00 usiku, jijini Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
Kardinali Pengo mwenye umri wa miaka 81 amefariki Dunia mara baada ya kuugua kwa muda mrefu ambapo kwa mara ya mwisho Askofu Mkuu wa sasa wa jimbo Katoliki la Dar es Salaam Jude Thadaeus Ruwa’ichi kwenye ibada ya mkesha wa Krismas alisema kuwa Pengo alipelekwa nchini India kwa ajili ya matibabu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotoka ofisi ya Askofu Mkuu wa jimbo la Dar es Salaam imeeleza kuwa taratibu za mazishi zitatangazwa mara baada ya mipango kukamilika.
ZINAZOFANANA
Mahakama yaamuru Wakazi kumlipa Mil 100 Baba Levo
Kongamano la Kimataifa la Utamaduni kufanyika Zanzibar Mei 2026
Rais wa FA ya Congo afungwa maisha jela