February 20, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Aliyemkamata mhamasishaji vurugu Mbeya atoa ushahidi kesi ya Lissu

Tundu Lissu akiwa mahakamani

 

SHAHIDI wa 15 kwenye kesi Na. 19605/2025 ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambaye ni askari wa Jeshi la Polisi aliyejitambulisha kuwa ni kuwa yeye ni G.9304 Amani (35), anayefanyakazi Mbeya mjini aliyemkamata mtuhumiwa wa kuhamasisha vurugu za uchaguzi mkuu 2025. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akiwa katika Mahakama Kuu, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, mbele ya jopo majaji watatu linaloongozwa na Jaji Dustan Ndunguru akishirikiana na Jaji James Karayamaha na Jaji Ferdinand Kiwonde, alitoa ushahidi wake akiongozwa na wakili wa serikali mkuu Nassoro Katuga, amedai kuwa tarehe 4 Aprili akiwa katika kituo cha Polisi Ilomba-Mbeya Mjini alipewa maelekezo na Inspekta Joram ya kwenda Isyesye mtaa wa Mwamtengule kwenda kumkamata dereva wa bodaboda anayehamasisha na kupanga njama za kufanya fujo na kuharibu uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Koplo Amani anadai kuwa alipewa ya askari mwenzake ambaye yupo kitengo cha intelijensia ili akamuoneshe watu waliokuwa wanapanga hizo njama.

“Askari ambaye yupo intelijensi ni askari wanaofanya kazi ya kujichanganya na wananchi ili wapate taarifa mbalimbali za uhalifu, tulivyokutana akaniongoza na kunionyesha mtuhumiwa ambaye nilipaswa kumkamata.’’

Amedai kuwa eneo la tukio kulikua na watu wengi lakini wao wakapita kwa siri na kuoneshwa mtuhumiwa katika kijiwe cha bodaboda akiwa na wenzake.

Koplo Amani ameendelea kueleza kuwa kuwa Baada ya kuonyeshwa mtu huyo, alimuita pembeni na kujitambulisha kuwa yeye ni askari na kwamba amekwenda kumkamata kutokana na tuhuma zake za kuhamasisha vurugu na kuharibu uchaguzi mkuu wa 2025.

Anadai kuwa baada ya kujitambulisha mtu huyo hajabisha kwenda kituo cha polisi hivyo akaenda naye kituo cha polisi cha Ilomba.

Kolpo Amani anasema kuwa mtuhumiwa huyo ni P3 ambaye ni sehemu ya mashahidi katika kesi hiyo ambaye alimhoji kama mtuhumiwa wa uchochezi na kuhamasisha kufanya vurugu na kuharibu uchaguzi mkuu wa 2025.

Akadai alimhoji kwa mujibu wa kifungo cha 390 cha sheria ya kanuni ya adhabu

“Baada ya kumhoji mtuhumiwa alinieleza kwamba ni kweli alihamasisha wenzake kufanya fujo na kuharibu uchaguzi mkuu wa 2025”

‘Pia alinieleza siku hiyo ya tarehe 4 April 2025 alikua akipitia taarifa mbalimbali na wakati anaendelea kupitia taarifa kwenye mtandao wa youtube alisikia mtu ambaye alimtaja kama Mwenyekiti wa Chadema anayeitwa Lissu akiongea na kutoa kauli za kuhamasisha uasi, kufanya vurugu na kuharibu uchaguzi mkuu wa 2025,” alidai Koplo Amani.

Koplo Amani: Baada ya kumaliza kumuandika maelezo nilimjulisha Inspekta Joram na akanipa maelezo kwamba mtuhumiwa adhamimiwe na aripoti kituo cha polisi Ilomba na aripoti kila baada ya siku tatu.

Wakili Katuga: Nini kilifanyika tarehe 17 Aprili 2025

Koplo Amani : Tarehe 17 Aprili 2025 nikiwa kituo cha polisi Ilomba nilipewa maelekezo na Inspekta Joram ya kuandika maelezo kama shahidi.

Wakili Katuga: Kingine?

Koplo Amani: Nilipewa maelekezo ya kumwandika kama shahidi kuhusiana na kile alichoeleza kwenye maelezo yake kwamba aliona mwenyekiti wake wa Chadema akihamasisha vurugu na kuharibu uchaguzi mkuu wa 2025 na kwamba baada ya kuona kauli ile yeye kama mfuasi wa Chadema , alihamasika kutokana na kauli zile na alikua tayari kuwashawishi vijana wenzake kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha kufanya vurugu na kuharibu uchaguzi mkuu wa 2025.

Wakili Katuga: Baada ya hapo?

Koplo Amani: Baada ya kumaliza kumuandika maelezo nilimjulisha Inspekta Joram.

Wakili Katuga: Ukafanya nini?

Koplo Amani: Hayo maelezo nilimkabidhi inspekta Joram.

Wakili Katuga: Waheshimiwa majaji ni hayo tu kwa shahidi huyu.

Itaendelea

About The Author

error: Content is protected !!