BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imeshiriki katika kilele cha maadhimisho ya miaka 30 ya Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) yaliyohitimishwa leo jijini Dar es Salaam, huku ikisisitiza dhamira yake ya kuongeza mchango na ushirikiano wake wa muda mrefu katika kupambana na saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake nchini. Anaripoti Mwandisbi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Akizungumza mbele ya Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Lameck Nchemba, aliyetembelea banda la maonesho la benki hiyo katika viunga vya maadhimisho hayo, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa NBC, Godwin Semunyu, alisema kwa kipindi cha miaka sita tangu kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya NBC na ORCI, benki hiyo imefanikiwa kuchangia zaidi ya shilingi milioni 800 kupitia mbio zake za hisani za NBC Dodoma Marathon.
Alifafanua kuwa fedha hizo zimewezesha kufanyika kwa uchunguzi (screening) wa saratani ya shingo ya kizazi kwa takribani wanawake 200,000 kote nchini, hatua iliyochangia kwa kiasi kikubwa kuokoa maisha na kuongeza uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa uchunguzi wa mapema.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu, kupitia programu hii ya uchunguzi tumewezesha pia matibabu kwa mamia ya wanawake waliogundulika kuwa na dalili au vimelea vya saratani hiyo, na wengi wao wamepata tiba, kupona na kurejea katika familia zao wakiwa salama,” alisema Semunyu.
Alisisitiza kuwa NBC itaendelea kuimarisha ushirikiano wake na ORCI pamoja na wadau wengine, kwa lengo la kuwafikia wanawake wengi zaidi, kuongeza huduma za uchunguzi na matibabu, na hivyo kuendeleza mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi nchini.
ZINAZOFANANA
Meridianbet yakupa Super Heli Premium, burudani na ushindi wa kiwango cha juu
Furahia Samsung A26 na Meridianbet leo
Taarifa zote za michezo njoo Meridianbet Sport Portal