KAMPUNI ya Airtel Tanzania leo imekabidhi zawadi ambazo ni Tv na Bajaji kwa washindi saba kupitia kampeni yake ya miezi mitatu ya Nyoosha mwaka na myairtelapp ikithibitisha dhamira yake ya kuwazawadia wateja wanaotumia huduma za kifedha kidijitali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Katika hafla ya makabidhiano ya zawadi iliyofanyika leo, washindi wamekabidhiwa runinga (TV) na bajaji zawadi zinazolenga kuboresha maisha na kufungua fursa za kwa watumiaji wa mtandao wa Airtel.
Kampeni hii inaendelea kuvutia ushiriki wa wateja kutoka maeneo mbalimbali nchini wanaotumia Airtel Money kwa miamala ya kila siku kama kutuma na kupokea fedha, kulipa bili na kufanya malipo kwa wafanyabiashara, sambamba na kununua muda wa maongezi.
Tangu kuzinduliwa kwake, kampeni ya Mwaka Umenyooka imegusa maisha ya wateja wengi kwa kutoa zaidi ya bajaji saba, zaidi ya runinga 30, bodaboda nane, pamoja na gari moja aina ya Mazida CX5 hadi sasa. Zawadi hizi zinaonyesha dhamira thabiti ya Airtel Money katika kuendeleza ujumuishaji wa kifedha kidijitali huku ikiwarudishia thamani wateja wake.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Edward Mtingwa, Meneja wa Thamani kwa Wateja wa Airtel, amesema kampeni hiyo imeundwa kuthamini uaminifu wa wateja huku ikihamasisha matumizi ya huduma za kifedha kidijitali zilizo salama na rahisi.
“Kupitia kampeni ya Mwaka Umenyooka, tunawapongeza na kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutumia Airtel Money katika miamala yao ya kila siku. Kampeni hii inaonyesha dhamira yetu ya kurudisha thamani kwa wateja wetu huku tukihamasisha matumizi ya huduma za kifedha kidijitali zilizo salama na rahisi,” alisema Mtingwa.
Mmoja wa washindi, Omary Kirungi, alieleza furaha yake baada ya kupokea runinga.“Nashukuru sana Airtel Money kwa zawadi hii. Sikutarajia kushinda, lakini sasa familia yangu itafurahia TV mpya nyumbani. Hii imenitia moyo kuendelea kutumia Airtel Money kwa miamala yangu ya kila siku,” alisema Kirungi.
Mshindi mwingine, Oscar Antony, pia alitoa shukrani zake baada ya kupokea zawadi yake.“Hii ni furaha kubwa kwangu. Zawadi hii itanisaidia sana katika maisha yangu ya kila siku. Nawashukuru Airtel Money kwa kutambua na kuthamini wateja wao,” alisema Antony.
Airtel Money inaendelea kujizatiti kutoa suluhisho za kifedha zilizo salama, za haraka na rahisi, zinazowawezesha watu binafsi na wafanyabiashara. Kampeni ya Mwaka Umenyooka inaendelea nchi nzima, ikitoa fursa zaidi kwa wateja kushinda kila wanapofanya miamala kupitia Airtel Money.
ZINAZOFANANA
TAMISA yawahamasisha vijana kuchangamkia fursa za uwekezaji katika sekta ya madini
Bei za mafuta zashuka maradufu kwa mwezi Februari
KESI ZA UCHAGUZI: Wako wapi Wanasheria wa SMZ?