Dk. Rugemeleza Nshala, Mwanasheria Mkuu wa Chadema
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimedai kuwa muda wa kisheria wa zuio la Mahakama Kuu wa kukizuia chama hicho kisifanye shughuli zake za kisiasa umekoma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Dk. Rugemeleza Nshala, amesema kuwa zuio hilo uhalali wake upo kisheria hivyo na imebatilika kwa mujibu wa sheria hiyo.
Dk. Nshala akirejea matukio ya juzi tarehe 21 Januari 2026, la Nkasi la Jeshi la Polisi kuwazuia wafuasi wa chama hicho wilaya hapo kuadhimisha miaka 33 ya chama chao kwa kupanda miti na kuzingira eneo lilipangwa kufanyika kwa maadhimisho hayo ingawa Polisi wenyewe walikana kufanya hivyo.
Tukio jingine ni lile la Mbeya Vijijini la jeshi hilo liliwavamia ofisi ya Chadema tawi la Inyala, ambapo viongozi wa Chadema walikuwa kwenye zoezi la kupandisha bendera nusu mlingoti kwa lengo ka kuombeleza msiba wa muasisi wa chama hicho Mzee Edwin Mtei.
Dk. Nshala anasema Polisi walivamia eneo hilo la kushusha bendera za chama kisha kuwakamata baadhi ya viongozi.
Mwanasheria huyo wa Chadema anasema kuwa kwa sasa Chadema kipo huru kufanya shughuli zake za kisiasa kwa kuwa sheria inatoa ukomo wa zuio.
Zuio hilo linatokana na kesi iliyofunguliwa na Saidi Mohamed Issa, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema Zanzibar, Ahmed Rashid Khamis na Maulidah Anna Komu wajumbe wa bodi ya wadhamini wa Chadema.
“Tunapenda kuwaeleza Watanzania wote na wapenda demokrasia, kuwa zuio la kufanya shughuli za kisiasa kwa Chadema lilikoma tarehe 10 Desemba 2025 ambayo ilikuwa ni mwezi wa sita kamili tangu zuio hilo lilipowekwa na Jaji Hamidu Mwanga tarehe 10 Juni 2025.
“Kukoma huko ni kutokana na Kanuni ya 3 ya Amri ya 37 ya Sheria ya Mwenendo wa Madai (Civil Procedure Code Act Cap 33 R.E. 2023) ambayo kwa tafsiri isiyo rasmi inasomeka kwa Kiswahili: Ikiwa ni Pamoja na masharti mengine ya kutunza hesabu na kutoa amana, Mahakama inaweza kutoa amri ya zuio kwa mujibu wa kanuni ya 1 au kanuni ya 2 na amri hiyo itakuwa na maisha kwa kipindi kilichotajwa na Mahakama, lakini kisichozidi miezi sita.”
Dk. Nshala ameongeza kuwa “Mkazo umeongezwa. 5. Kifungu hiki cha sheria kilitafsiriwa kwa utuo na Mahakama ya Rufaa ya Tanzania katika kesi ya African Trophy Hunting Ltd vs Attorney General and 4 Others (Civil Appeal 25 of 1997) [1998] TZCA 11 (3 Desemba 1998), ambapo Mahakama hiyo ya juu kabisa nchini ilisema kwa uwazi kabisa kuwa amri ya zuio inaweza kutolewa kwanza kwa miezi sita na inaweza kuongezwa zaidi lakini nyongeza hiyo ikiwa ni pamoja na zuio la kwanza lisizidi jumla ya mwaka mmoja. Kwa faida ya wote tunaomba kunukuu na kutoa tafsiri ya uamuzi huo muhimu.”
ZINAZOFANANA
Kesi ya Mwambe yapigwa kalenda, kusikilizwa Januari 26
Tundu Lissu asherehekea Birthday gerezani
AG Zanzibar aweka mapingamizi kesi za Uwakilishi