January 17, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Tume.yamtangaza Museven mshindi Urais Uganda

 

TUME ya uchaguzi nchini Uganda imemtangaza Rais Yoweri Kaguta Museveni kama mshindi wa uchaguzi uliofanyika Alhamisi wiki hii, akiwa na jumla ya kura 7,946,772 ambayo ni asilimia 71.65% ya kura zote zilozopigwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Uganda … (endelea).

Mpinzani wake wa karibu Robert Ssentamu Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine alikuwa wa pili, akiwa na jumla ya kura 2,741,238 au asilimia 24.72%.

Kwa mujibu wa tume hiyo, kura 11,366,201 zilipigwa katika uchaguzi huu wa mwaka 2026, ikiashiria asilimia 52.50% ya idadi ya wapiga kura waliojitokeza kushiriki.

Hata hivyo, kura 275,353 (2.42%) zilizopigwa zilikuwa batili.

Matokeo ya uchaguzi

Museveni 7,946,772 (71.65%)

Bobi Wine 2,741,238 (24.72%)

Bulira Frank 45,959 (0.41%)

Skip Iliyosomwa zaidi and continue reading Iliyosomwa zaidi Museveni

Rais Museveni atangazwa mshindi wa uchaguzi Uganda

Mwanamke

Sababu tatu za kutokwa na damu kwenye kinyesi

Kwa nini kuna maandamano Iran na Trump amesema Marekani itafanya nini?

Bobi Wine

Matokeo ya uchaguzi Uganda 2026: Bobi Wine yuko wapi?

End of Iliyosomwa zaidi

Kasibante Robert 33,440 (0.30%)

Joseph Mabirizi 23,458 (0.21%)

Mugisha Muntu 59,276 (0.53%)

Mubarak Munyagwa 31,666 (0.29%)

Nandala Mafabi 209,039 (1.88%)

Ushindi wa Museveni unamaanisha kwamba ataongeza muda wake wa miaka 40 madarakani kwa miaka mingine mitano.

Awali, mpinzani wake wa karibu Bobi Wine alikataa matokeo hayo, akiwataka raia wa Uganda kushiriki maandamano yasiyo ya vurugu.

Museveni, mwenye umri wa miaka 81, aliingia madarakani kwa mara ya kwanza mwaka 1986 kama kiongozi wa waasi lakini tangu wakati huo ameshinda chaguzi

About The Author

error: Content is protected !!