Meridianbet imeendelea kuthibitisha dhamira yake ya kugusa maisha ya watu kwa vitendo, kwa kuwekeza katika afya na ustawi wa mama wajawazito pamoja na wale waliojifungua hivi karibuni. Mpango huu wa kijamii ni endelevu na unalenga kutoa msaada wa moja kwa moja kwa akina mama wajawazito na waliojifungua, ili kuhakikisha wanapokea msaada unaohitajika.
Msaada uliotolewa unajumuisha mahitaji ya kila siku ya mama na mtoto, kama vile nepi, nguo za watoto wachanga, wipes, sabuni na taulo za kike. Vifaa hivi, ingawa ni vya kawaida, vina mchango mkubwa katika kuboresha usafi, afya na faraja, na kusaidia kupunguza mzigo wa gharama zinazowakabili akina mama katika kipindi cha uzazi.

Hatua hii ni sehemu ya mpango wa Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR) wa Meridianbet, unaotambua kuwa maendeleo ya biashara hayawezi kutenganishwa na ustawi wa jamii. Kampuni inaamini kuwa kusaidia makundi yenye uhitaji maalum ni njia bora ya kuendeleza jamii yenye afya, matumaini na ustawi endelevu.
Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi! Tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10#.
Akizungumza katika tukio hilo, Afisa Mawasiliano wa Meridianbet, Nancy Ingram, alisisitiza kuwa mafanikio ya kweli huonekana pale yanapogusa maisha ya watu wa kawaida. Alieleza kuwa msaada huu umetolewa kwa nia ya kuwapa akina mama nguvu na matumaini mapya wanapoanza safari ya malezi, huku wakipokea changamoto za kwanza za maisha ya familia.

Walengwa wa msaada huo walieleza shukrani zao, wakisema msaada umefika kwa wakati muafaka na utakuwa msaada mkubwa katika maisha yao ya kila siku. Kwa hatua hizi, Meridianbet inaendelea kujijenga kama mdau wa kijamii anayejali ustawi wa jamii, ikionyesha kwamba mafanikio ya kibiashara yanaweza kwenda sambamba na kugusa maisha ya watu kwa vitendo.
ZINAZOFANANA
Lucky Loser kukupa uhakika wa furaha hata ukipoteza
Kwa taarifa zaidi ingia Meridianbet Sport Portal
Kesi ya uhaini ya Lissu kusikilizwa siku 26 mfululizo