January 7, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Trump amuonya kiongozi wa muda wa Venezuela

 

RAIS Donald Trump amemuonya Rais wa muda wa Venezuela, Delcy Rodríguez, kwamba anaweza kukabiliwa na adhabu kali kuliko ya Maduro. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). 

Rais wa muda wa Venezuela Delcy Rodriguez ameunda tume ya kutaka kuachiliwa kwa Rais Nicolas Maduro na mkewe Cilia Flores ambao walikamatwa na Majeshi ya Marekani na kupelekwa Marekani.

Rodriguez alimteua kaka yake, Jorge Rodriguez, Rais wa bunge la kitaifa, na Waziri wa Mambo ya nje Yvan Gil kuwa Mwenyekiti Mwenza wa tume hiyo. Waziri wa habari Freddy Nandez pia atahudumu katika tume hiyo.

Akishutumiwa kwa ulanguzi wa dawa za kulevya, ugaidi na uhalifu mwingine, Maduro anatazamiwa kufika mbele ya hakimu huko Manhattan, New York, leo Jumatatu saa kumi na mbili jioni ili kujulishwa rasmi kuhusu mashtaka dhidi yake.

Trump pia alimuonya Rais wa Colombia, nchi jirani ya Venezuela, katika matamshi aliyoyatoa alipokuwa akipanda Air Force One, ndege iliyombeba Rais huyo wa Marekani.

About The Author

error: Content is protected !!