January 7, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Mwigulu afungua skuli ya Chukwani, Zanzibar

 

WAZIRI Mkuu Mwigulu Nchemba leo 5 Januari 2026 amefungua Skuli ya Sekondari Chukwani, Zanzibar ikiwa ni sehemu ya shamrashamra ya maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Anaripoti Zakia Nanga, Zanzibar … (endelea).

Ujenzi wa skuli hiyo ambayo imegharimu shilingi bilioni 6.1 imeanzishwa kwa lengo la kuwaandaa vijana wenye maarifa, ujuzi, ubunifu na maadili, kwa kuunganisha nadharia na vitendo na hivyo kuwa na manufaa mengi ikiwemo kuongeza fursa za elimu bora kwa watoto wa Zanzibar.

Mwigulu amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Hussein Mwinyi kwa uwekezaji mkubwa alioufanya katika sekta ya elimu.

About The Author

error: Content is protected !!