RAIS wa Venezuela, aliyeng’olewa mamlakani, Nicolás Maduro, tayari amefikishwa katika mahakama ya New York, nchini Marekani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Rais aliyeondolewa madarakani wa alikamatwa katika operesheni ya Marekani, juzi Jumamosi, kufuatia mashambulizi makubwa yaliyofanywa nchini mwake.
Mara baada ya shambuli hilo, Rais wa Marekani, Donald Trump alisema, taifa lake, limefanya mashambulizi yaliyolenga maeneo ya kijeshi mjini Caracas na sehemu nyingine za nchi hiyo, na kwamba Maduro hakushinda uchaguzi na kiongozi aliyejipachika madarakani.
Maduro amefika katika jengo la mahakama ya Manhattan, ambapo orodha kamili ya mashtaka dhidi yake inatarajiwa kusomwa.
Vyanzo vya taarifa vinasema, Maduro anatuhumiwa na Marekani kwa biashara haramu ya dawa za kulevya na makosa yanayohusu silaha, na kuendesha utawala wa “kigaidi wa dawa za kulevya,” madai anayokana.
Madai mengine, ni pamoja na kuwatesa, kuwateka na kuendesha magenge ya mauaji dhidi ya wapinzani wake wa kisiasa.

Mke wa Maduro, Cilia Flores pia naye alikamatwa katika operesheni hiyo na anatuhumiwa kwa rushwa.
Washirika wa kiongozi aliyeondolewa madarakani, ikiwa ni pamoja na China na Iran, wanaitaka Marekani kumwachilia huru.
Beijing inasema vitendo vya Washington ni “ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa.”
Katika uchaguzi mkuu wa 2024, María Machado mpinzani aliyekuwa na nguvu na kukabiliana na Maduro alizuiwa kugombea urais na Tume ya Uchaguzi (CNE).
Viongozi wengine wa upinzani waliokuwa na nguvu, akiwamo Freddy Superlano na Roberto Abdul, walikamatwa na kufungwa gerezani.
Wengine walikimbia nchi kunusuru maisha yao, akiwamo Edmundo González Urrutia na Leopoldo López. Walikimbilia Hispania na kumuacha Maduro kuwa mgombea pekee mwenye nguvu.
Akavikusanya vyama 13 vya upinzani na kutangaza kumuunga mkono.
ZINAZOFANANA
Wanafunzi 77 wafutiwa matokeo ya kidato cha nne, ufaulu wapanda
Uwekezaji wa Samia, wanafunzi 16 wasomea Data Science na AI Afrika Kusini
Meridianbet yawakumbuka wanaopitia maisha magumu Kinondoni