TANZANIA imeandika historia mpya kwenye michuano ya AFCON 2025. Ni baada ya kufuzu hatua ya 16 bora, kupitia nafasi ya timu bora zilizomaliza nafasi ya tatu. Hatua hiyo, imethibitisha kuwa safari ya Taifa Stars kwenye mashindano haya, haikuwa ya kushiriki tu, bali kushindana. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Katika historia ya AFCON, njia hii ya kufuzu si jambo geni kwa mataifa yaliyokuja kufanya makubwa. Benin, kwa mfano, waliwahi kufika hadi robo fainali mwaka 2019 licha ya kutoshinda mchezo hata mmoja kwenye hatua ya makundi.
Vilevile, Ivory Coast, mabingwa watetezi wa sasa, walipitia njia kama ya Tanzania kufuzu kama “best losers,” nafasi ya tatu kabla ya kuibuka mabingwa, jambo linaloonyesha kuwa nafasi hii si ya bahati bali ni fursa halali ya kujijenga na kusonga mbele.
Sikutarajia kwamba ingefuzu 16 bora, ni hatua kubwa”, anasema Amri Kiemba, nyota wa zamani wa Tanzania na mchambuzi wa soka.
Kwa Tanzania, kufuzu huku kunapata uzito zaidi kutokana na ukweli kwamba imefunga katika kila mchezo wa kundi, ikikusanya mabao matatu dhidi ya Nigeria, Uganda na Tunisia. Hii ni ishara ya maendeleo ya wazi, hasa ikizingatiwa kuwa Taifa Stars kwa muda mrefu ilihangaika kupata mabao kwenye mashindano makubwa.
ZINAZOFANANA
OMO agoma kuingia katika serikali ya Zanzibar
Tusua kibabe na Meridianbet mechi za leo
Ushindi upo nje nje siku ya leo na Meridianbet