WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, Mwigulu Nchemba, ameagiza wizara ya Uchukuzi, kuwachukulia hatua, watumishi wote wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), waliohusika na ubadhirifu wa kiasi cha Sh. 2.5 bilioni. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Akizungumza leo, tarehe 24 Desemba 2025, wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa kivuko eneo la Kigamboni, Mwigulu amesema, “…hawa watumishi, ni lazima wafukuzwe kazi mara moja.”
Ameongeza, “Serikali haitavumilia matumizi mabaya ya madaraka na ufujaji wa fedha za umma. Hapana. Tutachukua hatua na hapa lazima tonyeshe uwajibikaji.”
Amesema, vitendo vya ubadhirifu vimekuwa chanzo cha kudorora kwa huduma za usafiri wa vivuko na kuongezeka kwa gharama zisizo za lazima kwa serikali.

“Watu wasioweza kujirekebisha ni lazima warekebishwe. Kumekuwepo na matumizi mabaya ya madaraka na fedha, hali ambayo haiwezi kuvumiliwa,” alieleza waziri mkuu huyo.
Amesema, kwa sasa matengenezo yamesimama kwa baadhi ya vivuko kutokana na madeni ya takribani Sh. 800 milioni.
Amesema, taarifa za kifedha za TAMESA zinaonesha kuwa baadhi ya watumishi wa taasisi hiyo, wamehusika na ubadhirifu wa Sh. 2.5 bilioni.
Waziri mkuu Mwigulu ameonya kuwa endapo hatua kali hazitachukuliwa, serikali inaweza kujikuta ikitumia fedha nyingi katika matengenezo ya vivuko chakavu badala ya kununua vivuko vipya.
Kwa mujibu wa Mwigulu, hali hiyo, itasababisha kuongezeka mzigo kwa wananchi na kuathiri utoaji wa huduma muhimu kwa jamii.
ZINAZOFANANA
BAKWATA yapigwa mweleka mahakamani
2025, mwaka mchungu usiosahaulika
Jeshi la Polisi ni mwendo wa ‘kukanusha’