Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, amesema Serikali inajiandaa kuanza utekelezaji wa mageuzi makubwa ya mfumo wa elimu yatakayobadilisha muundo uliodumu kwa zaidi ya nusu karne. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 10 Desemba 2025, katika Kituo cha Urithi wa Ukombozi jijini Dar es Salaam, Profesa Mkenda amesema mfumo wa sasa wa 7+4+2+3+ ulianza kutumika kati ya mwaka 1965 na 1968 chini ya uongozi wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Amesema chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, Serikali inakuja na mfumo mpya wa 6+4+2/3+3+, ambao utaifanya elimu ya msingi kuwa miaka sita badala ya saba.
Mfumo huo pia utaanzisha elimu ya lazima ya miaka 10, tofauti na mfumo wa sasa wenye miaka saba.
Kwa mujibu wa Profesa Mkenda, utekelezaji wa mwanzo umeanza kupitia mitaala mipya kwa wanafunzi wa darasa la tatu ambao ifikapo mwaka 2027 watakuwa wa kwanza kufikia darasa la sita na kufanya mtihani wa kupima uwezo kabla ya kuendelea moja kwa moja na elimu ya sekondari ya kati hadi kidato cha nne.
Utekelezaji rasmi wa mfumo mpya kitaifa unatarajiwa kuanza mwaka 2028.
ZINAZOFANANA
Shule za sekondari, Veta kufungiwa miundombinu ya nishati safi ya kupikia
Wanafunzi 937,581 wachaguliwa kujiunga kidato cha kwanza, wasichana vinara
Watahiniwa 937,581 wafaulu elimu ya msingi