MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachilia huru mfanyabiashara Jennifer Jovin maarufu kama Niffer (26) na Mika Chavala ( 32) baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka kuamua kutoendelea na kesi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Niffer alikamatwa tarehe 24 Oktoba ambapo tangu ashikiliwe mpaka kufika leo anaachiwa huru zinatimia siku 40 .
Mahakama imefikia uamuzi huo leo Jumatano tarehe 3 Desemba 2025 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Aaron Lyamuya baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuwasilisha hati inayoitwa Nolle Prosequi ( taarifa ya kutokuwa na nia ya kuendela na mashtaka dhidi ya washtakiwa) kwa mujibu wa kifungu cha 92(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai marejeo ya mwaka 2023″.
Kifungo hicho kinampa mamlaka DPP kuamua kuachana na kesi yoyote ya jinai muda wowote isipokuwa wakati wa hukumu.
Mapema Wakili wa Serikali, Titus Aron alidai shauri hilo leo liliitwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa, lakini DPP kwa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 92(1) cha Mwenendo wa Mashauri ya Jinai CPA hana nia ya kuendelea kuwashitaki washitakiwa wote wawili.
“Hivyo kwa mamlaka hiyo aliyoanayo chini kifungu tajwa ameamua kuwaondolea mashitaka washitakiwa wote wawili,” alisema Titus.
Baada ya kuelezwa hayo Wakili wa Utetezi, Peter Kibala alidai wamesikia na hawana pingamizi katika hilo kwakuwa ndiyo sheria inavyoelekeza, hivyo alidai anaiomba mahakama iweze kutamka kwamba washtakiwa wameachiwa.
Hakimu Lyamuya aliwaeleza washitakiwa kuwa upande wa mashitaka umewasilisha ombi ya kuwafitia mashitaka chini ya kifungu kilichotajwa, hivyo Mahakama inakubali ombi hilo na kueleza imewaachia huru washtakiwa isopokuwa kama watashikiliwa kwa jambo jingine.
Washtakiwa hao wanakuwa ni miongoninwa wsshitakiwa 1736 wanaoondolewa mashitaka na kuachiwa kati ya 2045 waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhaini mahakamani kutokana na vurugu ziliotokea Oktoba 25,mwaka huu.
Washtakiwa hao wameachiwa kufuatia msamaha wa Rais Samia Suluhu Hassan alioutoa Novemba 13,2025 wakati akihutubia Bunge mkoani Dodoma kwa mara ya kwa baada ya serikali ya awamu ya sita kuingia madarakani.
ZINAZOFANANA
Rais Samia: Tulitumia nguvu inayostahili, walitaka kufanya mapinduzi
Samia: Oktoba 29 walitaka kupindua dola ninayoiongoza
TANESCO yakanusha kuhusika na shambulio la Dk. Kitima