ALIYEWAHI kuwa Katibu wa Mwalimu Nyerere, Mzee Kasori, amekosoa kufanyika kwa mkutano kati ya Rais Samia na wanaoitwa, “Wazee wa Dar es Salaam.” Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Akiandika kupiti mitandao ya kijamii, Kasori anasema yafuatayo:
Ndugu watanzania wenzangu.
Salaam.
Nimesoma mitandaoni kuwa Mkuu wa Mkoa wa DSM,ndg Albert Chalamila amewahimiza Wananchi kumsikiliza Rais wa JMT Mhe.SAMIA atakapohutubia wazee wa DSM kesho tar.02/12/2025.
Binafsi nina mashaka iwapo Rais wetu ameshauriwa vema kuhusu hatua hii muhimu kwa sababu zifuatazo:-
Mosi, Wazee wa DSM ni akina nani na wanateuliwaje ili waalikwe ?
Kumbukumbu zangu na kama sikosei ni kwamba Wakati wa awamu ya kwanza, Mwl.J.K Nyerere alipenda kuzungumza na Watanzania kupitia kwa wazee wa DSM kutokana na sababu kuu tatu.
Kwanza, wazee wa Dsm kufuatia na uwepo wa Ofisi Kuu ya TAA na baadaye ya TANU ndiyo walioongoza harakati za kudai uhuru kutoka kwa Waingereza.
Pili,DSM ndiyo ilikuwa Makao Makuu ya nchi Kiserikali na ya Chama tawala, TANU .
Tatu,nchi ilikuwa chini ya mfumo wa Chama kimoja TANU na hatimaye CCM.
Kwa hiyo*** kwa mazingira ya sasa mimi siamini kwamba ni sahihi kwa Rais wa JMT kuendelea kutumia watu wanaoitwa wazee wa DSM ambao kiuhalisia ni wazee wa CCM***
Sababu ya pili ni kwamba,CCM tofauti na vyama vingine kama CHADEMA, ACT WAZALENDO na CUF haina Jumuiya ya Wazee kwa sababu ambazo hapa siyo mahala pake mimi kufafanua zaidi.
Hata Jumuiya ya Wanawake ya CCM bado inaitwa UWT jina ambalo lilikuwa sahihi wakati wa mfumo wa chama kimoja.
Kwa sasa ilitakiwa kuitwa UW-CCM kama ilivyo UVCCM.
UWT inaendana na chama kama TADEA ***.
Sababu ya tatu ni kuwa Makao makuu ya nchi kwa sasa ni DODOMA kwa hiyo iwapo ni lazima Rais wa JMT ahutubie wazee basi ni busara wawe ni wazee wa jiji la DODOMA ambayo ndiyo Makao Makuu ya nchi yetu ya Tanzania.
Sababu yangu ya nne ambayo ni kubwa zaidi ni kwa*** Rais anapotaka kueleza mambo ambayo yanayogusa maslahi au wajibu wa Wananchi wote anafanya hivyo kwa mujibu wa madaraka yake chini ya Katiba ya JMT—yaani Mkuu wa Nchi, Mkuu wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.
*** Kamwe Hafanyi hivyo akiwa ni Mwenyekiti wa CCM***
Kwa misingi hiyo,***washau
ri wa Rais SHURTI wajielekeze ipasavyo katika kumshauri kiongozi wetu mkuu ili kulinda kwa wivu mkubwa hadhi na heshima ya ofisi yake****
Kwa masilahi ya Taifa letu la Tanzania nawasilisha tafadhali.
Mzee Kasori S H
Katibu Msitaafu wa Mwalimu J K Nyerere
Jumatatu 01.12.2025
Saa 03.22 Usiku
ZINAZOFANANA
Dk. Kitima afunguka mazito, aeleza alivyovamiwa
Vijana wa kike wanachangia asilimia 80 ya maambukizi ya vvu
Tujihadhari na vurugu, tupate maendeleo – Mwigulu