PUMA Energy imemtangaza mshindi wa droo ya vilainishi, ambapo Boaz Aywayo ameibuka na Elite Card yenye thamani ya shilingi milioni 5 ambayo itamuwezesha kufanya manunuzi ya vilainishi au gesi katika kituo chochote cha Puma nchi nzima. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Mbali na zawadi hiyo kuu, droo hiyo pia ilizawadia washindi wengine vilainishi na fedha taslimu kama sehemu ya kampeni ya kuwashukuru wateja wa Puma Energy.
Akizungumza wakati wa makabidhiano, Mkuu wa Kitengo cha Oili Puma Energy, Matiko Bugumia, alisema droo hiyo ni sehemu ya mpango wa kampuni kuongeza thamani kwa wateja wake na kuendelea kuhimiza matumizi ya vilainishi halisi.
“Soko limekua kwa kasi, lakini changamoto ya bidhaa bandia bado ipo. Ndiyo maana Puma Energy inaendelea kutoa bidhaa bora na salama ili kulinda magari na vifaa vya wateja wetu,” alisema Matiko.

Puma Energy imekuwa ikiwekeza katika kupanua upatikanaji wa huduma zake pamoja na kuelimisha watumiaji kuhusu umuhimu wa kutumia vilainishi halisi vinavyotolewa na vituo rasmi vya mafuta, ili kuepuka athari za bidhaa bandia zinazoongezeka sokoni.
Kwa upande wake, mshindi wa droo, Boaz Aywayo, alishukuru Puma Energy kwa kampeni hiyo na akatoa rai kwa wateja wengine kununua bidhaa kwenye vituo vinavyoaminika.
“Bidhaa bandia ni changamoto, lakini Puma Energy imethibitisha kuwa chanzo cha bidhaa salama na zilizothibitishwa,” alisema.
ZINAZOFANANA
Meridianbet yazidi kutoa faraja, hospitali ya Ndumbwi yapata msaada muhimu
Muda wa kucheza Gates of Halloween umewadia, ni ushindi mikononi mwako
Naga Games kuleta burudani isiyokoma na ushindi kubwa ndani ya Meridianbet