Meridianbet imeendelea kuthibitisha nafasi yake kama kampuni inayoongoza si tu katika burudani na michezo ya kubahatisha, bali pia katika uwekezaji wa kijamii kupitia hatua yake mpya ya kugawa msaada wa chakula kwa familia zenye uhitaji jijini Dar es Salaam. Tukio hili limejenga picha halisi ya dhamira ya kampuni kuchangia maendeleo ya jamii kwa vitendo vinavyoleta mabadiliko ya moja kwa moja.
Katika mpango wake wa Corporate Social Responsibility (CSR), Meridianbet imejikita katika kuhakikisha kuwa kaya zinazopitia changamoto za kiuchumi zinapata msaada wa kuimarisha ustawi wao. Kampuni imetoa mahitaji muhimu ya kila siku kama mchele, unga, mafuta, sukari, sabuni na bidhaa nyingine za msingi zinazoweza kuwa msaada kwa kaya hizo.
Kwa mujibu wa mwakilishi wa kampuni, utekelezaji wa mradi huu ni sehemu ya mkakati mpana wa Meridianbet wa kuonyesha uwajibikaji wa kijamii kwa vitendo. “Tunafanya kazi kwa karibu na jamii, na kila mara tunapogundua pengo linalohitaji msaada, tunachukua hatua. Dhamira yetu ni kuendelea kuwa mshirika anayegusa maisha ya watu kwa njia endelevu, na msaada huu wa chakula ni moja ya hatua nyingi tunazoendelea kuchukua,” alisema.
Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi! Tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10#.
Wananchi waliopokea msaada huo walionyesha hisia za faraja na shukrani, wakieleza kuwa msaada huo umefika katika kipindi ambacho hitaji la mahitaji ya msingi limekuwa kubwa zaidi. Wengi walisisitiza kuwa msaada huo umeleta unafuu na kuwapa nguvu ya kupambana na changamoto za maisha katika mazingira ya kiuchumi yasiyoelezeka.
Meridianbet, ambayo imejijengea historia ya kuunga mkono jamii katika maeneo mbalimbali nchini, imeendelea kuwekeza katika miradi inayolenga afya, elimu, mazingira, michezo na ustawi wa makundi maalum kama watoto yatima na wagonjwa. Kupitia msaada huu mpya, kampuni imeonyesha kwa mara nyingine kwamba mafanikio yake yanaendana sambamba na kurudisha kwa jamii.
ZINAZOFANANA
Piga *149*10# kushinda Samsung A26 na Meridianbet
TVBET kukupa michezo mubashara ndani ya Meridianbet
Meridianbet yaipa kasino mtandaoni uso mpya na Aspect Gaming & Superspade Games