November 18, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Rais Samia aunda Tume ya kuchunguza matukio ya 29 Oktoba

 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameunda Tume Huru ya Uchunguzi itakayochunguza matukio yaliyotokea siku ya uchagazi mkuu tarehe 29 Oktoba yaliyoitwa na serikali matukio ya uvunjifu wa amani. Anaripoti Joyce Ndeki, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 18 Novemba 2025 na Katibu Mkuu Kiongozi, Moses Kusiluka kupitia taarifa rasmi ya Ikulu na ameteua wajumbe wakusimamia tume hiyo

Katika uteuzi huo, Rais Samia amewateua Jaji Mohamed Chande Othman jaji mkuu mstaafu wa mahakama ya Tanzania kuwa mwenyekiti wa tume ya uchunguzi Profesa Ibrahim Juma jaji mkuu mstaafu wa mahakama ya Tanzania.

Wajumbe wengine kwenye tume hiyo ni Balozi Ombeni Sefue mwanadiplomasia na katibu mkuu kiongozi mstaafu, Balozi Radhia Msuya mwanadiplomasia na balozi mstaafu, Balozi Lt. Gen. Paul Meela mwanadiplomasia na Balozi mstaafu, Said Mwema, mkuu wa jeshi la polisi Tanzania mstaafu.

Pia, Balozi David Kapya, Balozi mstaafu pamoja na Stergomena Tax aliyewahi kuwa katibu mtendaji wa jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) kuwa wajumbe wa Tume hiyo .

Hata hivyo wakosoaji wanadai kuwa tume hiyo haitakuja na jambo jipya kwa kuwa wajumbe wote wanatokana na serikali na hakuna mjumbe hata mmoja aliyetoka kwa wananchi.

About The Author

error: Content is protected !!