JOHN Heche, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Demokrasia), amesema kuwa viongozi wa chama hicho hawakuachiwa kwa dhamana kutoka mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa sababu ya mazungumzo ya maridhiano na serikali. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Heche ametoa kauli hiyo leo, tarehe 11 Novemba, 2025 muda mchache baada ya kuripoti katika kituo cha Polisi kikuu kama walivyotakiwa kufanya hivyo walipopewa dhamana jana tarehe 10 jioni katika kituo cha polisi cha Osterbay .
Heche amesema kuwa kuachiwa na kudhaminiwa kwao sio zao la mazungumzo yoyote kwa kuwa hawafanya jambo lolote.
“Tumeachiwa kama tulivyokamatwa, hatujazungumza chochote kuna propaganda kuwa tumetolewa kwa sababu ya mazungumzo hatujafanya mazungumzo yoyote,” amesema Heche.
Heche alikamatwa tarehe 22 Oktoba, 2025 kwenye ‘geti’ la mahakama kuu masjala ndogo ya Dar es Salaam huku viongozi wengine Amani Golugwa, naibu katibu mkuu wa Chadema, Godbless Lema mjumbe wa kamati kuu, na Boniface Jacob, Mwenyekiti wa Chadema kanda ya Pwani walikamatwa tarehe 8 Novemba.
ZINAZOFANANA
TRA yawataka wanachama wa SACCOS kuhamasisha ulipaji kodi
Mwanasheria wa kimataifa ataka Tanzania isifukuzwe Jumuiya ya Madola
Mwabukusi amuonya RC Chalamila, amtaja sakata la 29 Oktoba