November 8, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Gwajima vigogo Chadema wasakwa na Polisi

 

JESHI la Polisi nchini limesema kufuatia uchunguzi na ushahidi uliokusanywa hadi sasa kuhusu vurugu zilizotokea tarehe 29 Oktoba 2025, linawasaka kwa ajili ya kuwakamata baadhi ya vigogo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).

Watu wanaosakwa na Polisi ni Askofu Josephati Gwajima, Brenda Jonas Rupia, John Mnyika, Godbless Lema, Machumu Maximillian Kadutu (Askofu Mwanamapinduzi), Deogratius Mahinyila, Boniface Jacob, Hilda Newton, Award Kalonga na Amaan Golugwa.

Taarifa iliyotolewa usiku wa tarehe 7 Novemba 2025 na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, imesema Jeshi la Polisi linawataka watu hao kujisalimisha katika vituo vya Polisi mara moja watakapoona taarifa hii popote pale walipo.

“Pamoja na kwamba baadhi ya waliopanga na kutekekeza uhalifu huo wamekamatwa na kuanza kufikishwa mahakamani, Jeshi la Polisi nchini kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama linaendelea na msako mkali wa kuwatafuta wale wote waliopanga, kuratibu na kutekeleza uovu huo.

“Wakati hatua hizo zikiendelea Jamii inaombwa kuendelea kutoa ushirikiano wa dhati katika kutoa taarifa za Watu wote waliohusika ili hatua sahihi za kisheria zichukuliwe dhidi yao,” imeeleza taarifa hiyo.

About The Author

error: Content is protected !!