RAIS Samia Suluhu Hassan, amemwapisha Hamza Johari kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG). Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Johari ameapishwa leo Jumatano, tarehe 5 Novemba 2025, katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino, jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais, Dk Emmanuel Nchimbi.
Johari aliteuliwa tarehe 3 Novemba 2025, saa chache baada ya Samia kuapishwa kuwa Rais
Mwanasheria huyo ameapishwa kuendelea na wadhifa huo aliokuwa akiushikilia tangu alipoteuliwa kwa mara ya kwanza tarehe 15 Agosti 2024 kuchukua nafasi ya Dk Eliezer Feleshi aliyeteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
ZINAZOFANANA
Maswali tata ya Wahariri kwa Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba
Vyombo vya habari vimesifiwa au vimedhihakiwa?
Heri ya siku ya kuzaliwa kwa Polepole, ni siku 51 tangu ametekwa