October 21, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Wanafunzi 1.5 mil wa darasa la nne kuanza mtihani kesho

Katibu Mtendaji wa NECTA, Prof. Said Mohamed

 

JUMLA ya wanafunzi wa darasa la nne waliosajiliwa mwaka huu 1,582,140, wanatarajia kufanya mtihani wa upimaji wa kitaifa tarehe 22 hadi 23 Oktoba 2025 ambapo kati ya hao wavulana 764,290 Sawa na asilimia 48.31 huku wasichana wakiwa 817,850 Sawa na asilimia 51.69. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 21 Oktoba 2025 Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (NEKTA), Prof. Said Ally Mohamed amesema wanafunzi wapatao 1,475,637 Sawa na asilimia 93.27 watafanya upimaji kwa lugha ya kiswahili huku wanafunzi 106,503 sawa na asilimia 6.73 watafanya kwa lugha kiingereza.

Hata hivyo amebainisha kuwa wanafunzi 5,750 wenye mahitaji maalumu kati yao wenye uoni hafifu ni 1,164, na wasioona 111 wenye uziwi 1,161 wenye ulemavu wa akili 1,641 na wenye ulemavu wa viungo 1,673.

Katibu Mtendaji amesisitiza kuwa upimaji wa kitaifa wa darasa la nne ni muhimu kwa kuwa huwezesha kufahamu viwango cha wanafunzi katika kumudu stadi za juu za kusoma ,kuandika na kuhesabu.

Hata hivyo maandalizi yote yamekamilika ikiwa ni pamoja na kusambaza kwa karatasi za upimaji pamoja nyaraka zote muhimu zinazohusu upimaji huo katika halmashauri au manispaa zote nchi nzima wasimamizi wote wameshapewa semina na vituo vimekamilika vyote.

Aidha kamati zote za mitihani ziweke mikakati ya kuzuia mianya yote inayoanza kusababisha kutokea kwa udanganyifu na wasimamizi wote walioteuliwa kufanya kazi kwa umakini na kuzingatia uadilifu wa hali ya juu.

About The Author

error: Content is protected !!