
RAIS mstaafu wa Marekani, Barack Obama amemtaja aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga kama shujaa aliyepigania demokrasia sio tu nyumbani kwake – Kenya, bali kote barani Afrika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kenya … (endelea).
Katika ujumbe wake wa risala ya rambi rambi kwa wakenya, Obama alimkumbuka Odinga kama mtoto wa juhudi za kupigania uhuru wa nchi hasa ambaye baba yake alifungwa na serikali ya mbeberu kwa ajili ya kutaka Kenya kuwa huru mwaka 1952.
“Mara kwa mara nilipokutana naye, nilishuhudia akiweka taifa mbele ya haja zake za kibinafsi. Na kama viongozi wengine duniani alikuwa tayari kufuata barabara ya kutaka maridhiano na upatanisho hata baada ya muda mgumu,” ameeleza Obama katika ujumbe wake.
Obama ambaye ana asili ya Kenya alikozaliwa baba yake Hussein Obama, anamkumbuka Raila kwa jinsi alivyompa mapokezi mazuri alipofika nchini Kenya katika awamu ya kwanza ya uongozi wa Mwai Kibaki, akiwa Seneta wa Jimbo la Illinois
Raila aliandamana na Rais Obama kuelelea Kogelo kwa boma la babu yake alikoishi nyanya yake Sarah Obama alipokuwa akiishi.
Obama ambaye alikutana na kushirikiana na Odinga hasa alipokuwa Waziri Mkuu wa Kenya anasema, “maishani mwake, Raila alitoa mfano mkubwa sio tu kwa Wakenya na barani Afrika, bali duniani pia.
“Ninajua wengi watamkosa na kumbuka kwa dhati. Michelle nami tunatuma risala zetu za rambi rambi kwa familia yake na raia wa Kenya,” alieleza kwa njia ya masikitiko.
ZINAZOFANANA
Mambo matano makubwa kuhusu Raila
Raila Odinga ‘awasili’ Kisumu
TMA yatangaza utabiri wa mvua za msimu