
LEO Vodacom Tanzania PLC kwa ushirikiano na Bolt, Kampuni inayotoa huduma za usafiri kwa njia ya mtandao, wamezindua huduma mpya inayowapa wateja thamani zaidi katika kila safari wanayofanya, kupitia Tuzo Points, wateja wa Vodacom sasa wanaweza kutumia pointi walizopata kupata punguzo la bei kwenye safari za Bolt wakileta pamoja nguvu ya teknolojia, urahisi wa usafiri, na maisha ya kila siku yenye thamani zaidi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
“Dhamira yetu Vodacom daima imekuwa kuwaunganisha Watanzania kwa ajili ya mustakabali bora,” alisema Joseph Njuu, Meneja Usimamizi wa thamani ya wateja kutoka Vodacom Tanzania na kuongeza; “Ushirikiano huu na Bolt ni uthibitisho wa dhamira hiyo tunaleta suluhisho rahisi, linalowawezesha wateja na kuwazawadia kwa safari zao za kila siku.”
Kupitia ushirikiano huu, wateja wa Vodacom sasa wanaweza kutumia Tuzo Points zao ambazo hapo awali zilitumika kupata muda wa maongezi au bando za intaneti kulipia safari za Bolt kwa punguzo la bei. Huduma hii ni rahisi kutumia, ya kisasa, na imeundwa mahsusi kwa ajili ya Mtanzania wa leo anayethamini urahisi, uunganisho, na thamani katika maisha yake ya kila siku.
Milu Kipimo, Meneja wa Nchi (Country Manager) wa Bolt Business kwa Tanzania, Ghana na Afrika Kusini, alisema:
“Kushirikiana na Vodacom kunafungua milango zaidi ya fursa za kiuchumi na masoko. Kwa kuunganisha nguvu za kampuni inayoongoza katika mawasiliano nchini na jukwaa linaloongoza katika huduma za usafiri wa biashara, tutawezesha wakazi wa mijini, wajasiriamali, na wataalamu kuongeza tija katika kazi zao jambo litakalochochea ukuaji wa uchumi.”
Wateja wa Vodacom hupata Tuzo Points kiotomatiki kila wanapoongeza bando au kufanya miamala kupitia M-Pesa. Pointi hizo zinaweza kuonekana kupitia App ya M-Pesa au kwa kupiga *149*01#. Ili kutumia pointi hizo kupata punguzo kwenye safari za Bolt, mteja atachagua chaguo la “Tumia Tuzo Points kwa Bolt”, na kisha atapokea nambari ya punguzo (promo code), na kuingiza nambari hiyo kwenye Bolt App wakati wa malipo.
Kadri Vodacom inavyoendelea kusherehekea miaka 25 ya kuwaunganisha Watanzania, ushirikiano huu na Bolt unaendeleza dhamira yake ya kujenga jamii iliyounganishwa kupitia teknolojia jamii ambayo maisha yake yanakuwa bora zaidi kutokana na ubunifu.
ZINAZOFANANA
Dau lako na fursa ya ushindi wa Samsung A26 mpya kutoka Meridianbet
Slotopia, mtoa huduma mpya aliyeleta mzuka mpya Meridianbet.
Meridianbet yaunga mkono michezo, yadhamini “Chanika Veteran Bonanza 2025”