
John Mnyika, Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema
WAJUMBE wawili wa Bodi ya Wadhamini CHADEMA-Zanzibar, Ahmed Rashid Khamis na Maulida Anna Komu pamoja na Makamu Mwenyekiti Mstaafu, Said Issa Mohamed, wameiomba Mahakama Kuu itoe amri ya kuwakamata na kuwashikilia Viongozi wa CHADEMA, akiwemo Makamu Mwenyekiti John Heche na Kaimu Katibu Mkuu John Mnyika kwa madai ya kukiuka amri ya Mahakama. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kwa mujibu wa taarifa, wengine wanaotakiwa kukamatwa na kufungwa ni Rose Mayemba, Brenda Rupia, Hilda Newton, Twaha Mwaipaya na Gervas Lyenda.
Wajumbe hao Wameomba kibali hicho wanawatuhumu Viongozi tajwa wa CHADEMA kuwa wamekiuka kwa makusudi amri za Mahakama katika shauri la madai namba 8960 ya mwaka 2025 lililotolewa Juni 10, 2025 lililowataka wasijihusishe na masuala ya Siasa hadi Kesi ya Msingi itakapoamriwa.
Maombi hayo yamewasilishwa mbele ya Jaji Hamidu Mwanga.
ZINAZOFANANA
THRDC yapendekeza maridhiano kufanyika kabla ya uchaguzi
JWTZ yaonya wanaojaribu kulihusisha na siasa
Zitto awapigia magoti wananchi wa Kigamboni kumchagua Mndeme