
JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesema kuwa kumekuwepo na ongezeko la watu wanaotumia mitandao ya kijamii kuchapisha maudhui yanayochochea kuliingiza jeshi hilo katika mambo ya kisiasa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa habari na Uhusiano Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kanali Benard Masala Mlunga baadhi ya hoja hizo zinatolewa na watu waliopo katika mazingira ya kijeshi, wengine wakijinasibisha na JWTZ bila uhalali,na baadhi yao ni wale walioachishwa jeshi kutokana na tabia na mwenendo usiofaa au kujihusisha na siasa na uanaharakati.
JWTZ limeeleza kuwa linaendelea kutekeleza Majukumu yake kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uaminifu, utii na uhodari, likizingatia kiapo chake.
ZINAZOFANANA
THRDC yapendekeza maridhiano kufanyika kabla ya uchaguzi
Mahakama yaombwa kibali cha kuwakamata Viongozi wa Chadema
TCU yaongeza siku nne za udahili